Wednesday, August 27, 2014

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika amekamilisha ziara yake mkoani MbeyaWaziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa  Eng. Christopher Chiza, amekamilisha ziara ya siku tatu katika mkoa wa Mbeya . Katika ziara hiyo alipata fursa ya kutembelea miradi ya umwagiliaji ya bwawa la Lwanyo na Lyendwa.
Aidha alikagua maendeleo ya ununuzi wa mahindi unaofanywa na Wakala wa Taifa ya Hifadhi ya Chakula ( NFRA) katika wilaya ya Mbozi.
Mheshimiwa anategemea kurudi  Dar es Salaam leo.

Tuesday, August 26, 2014

Wilayani Mbozi mkoani MbeyaWaziri  wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa Eng Christopher Chiza, leo  anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani  Mbeya  ambapo  atatembelea  Wilaya ya Mbozi kukagua maendeleo ya ununuzi  wa mahindi unaofanywa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula ( NFRA) wilayani humo.
Pia  atatembelea bwawa la Lyendwa  ili kujionea hali halisi pamoja na kukagua  maendeleo ya ujenzi wa miundo mbinu ya umwagiliiani wilayani humo.

Waziri awashauri Halmashauri kushirikiana na sekta binafsi

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika mhe. Eng Christopher Chiza, awashauri  Halmashauri za Wilaya ya Mbarali kushirikiana na sekta binafsi kutatua changamoto za fedha zinazowakabili.  Aliongea hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Kilimo na umwagiliaji Igurusi  Wilayani Mbarali, Mbeya.
Aidha, Mhe.  Chiza ameainisha  taasisi  kama vile ANSAF, HELVATUS, Bill & Melinda  Gates  Foundation  ambazo zimekuwa na mchango mkubwa  katika kukuza sekta ya Kilimo nchini. 
Hivyo, alitoa wito kwa  Halmashauri za Wilaya kubuni vyanzo vingine vya fedha badala ya kutegemea Serikali pekee.


Waziri atoa agizo kwa WakulimaWaziri wa Kilimo Chakula na Ushirika mhe. Eng Christopher Chiza  leo amewataka Wakulima wa kijiji cha  Ukwile kata ya Isandula Wilaya ya Momba kutumia fursa ya mipaka ya nchi za jirani kama Malawi na Zambia katika kupata masoko ya mazao. Ushauri huo ameutoa baada ya kupokea taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Momba Mheshimiwa  Abihudi Saideya kwamba wakulima wamevuna ziada ya mazao ya mahindi na mtama lakini wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa soko la uhakika.

Mbarali kuunda timu ya WataalamuWaziri wa Kilimo Chakula na Ushirika mhe. Eng Christopher Chiza ameagiza kuundwa kwa timu ya wataalamu itakayo chunguza sababu za kubomoka kwa bwawa la Lwanyo lililopo katika kata ya Igurusi  Wilayani Mbarali.
Mradi wa bwawa  hilo umeshaigharimu Serikali takribani shilingi billion 3, ambapo baada ya kukamilika kwa ujenzi litawanufaisha  wananchi zaidi ya elfu sita ambao  wanaishi katika vijiji vitatu.
Aidha, timu hiyo itatakiwa kuchunguza kuanzia ubunifu wa mradi, utaratibu wa manunuzi,  jinsi alivopatikana Mkandarasi na aliyekuwa anaidhinisha malipo ya kugharimia ujenzi wa bwawa hilo.

Monday, August 25, 2014

Watendaji wa Halmashauri watakiwa kushikiri utekelezaji wa Mpango wa matokeo Makubwa SasaWaziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa Christopher K. Chiza amewataka Watendaji wa Halmashauri ya Mbarali kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mpango wa matokeo Makubwa Sasa (BRN).  Mheshimiwa Waziri alitoa wito huo katika ziara yake Wilayani humo, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Gulla Hussein.
Aidha, Mhe. Chiza ametoa wito kwa Wakulima kuwa mstari wa mbele katika kutafuta taarifa zinahusu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ili waweze kushiriki kikamilifu katika kufanikisha utekelezaji wake na hivyo kujiletea maendeleo ya haraka.