Thursday, September 18, 2014

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa Eng. Christopher Chiza akiangalia takataka  zilizokuwa kwenye magunia ya mahindi yaliyokuwa yameletwa na wafanyabiashara na wakulima kwa ajili ya kuyauza katika kituo cha NFRA- Dodoma

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa Eng. Christopher Chiza akizungumza na kujibu kero za wafanyabiashara na wakulima waliopeleka mahindi NFRA-Dodoma  kwa ajili ya kuyauza 

Mahindi yaliyonunuliwa na kituo cha NFRA-Dodoma yakipangwa kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Friday, September 12, 2014

TIMU YA KILIMO SPORTS CLUB YAKABIDHIWA JEZIMhandisi Rajabu Mtunze amepokea jezi  kwa niaba ya Mheshimiwa  Waziri wa  Kilimo Chakula na Ushirika kutoka Kampuni ya Savoy Farm Limited. Kampuni ya Savoy Farm Limited imeingia makubaliano na kusaini mkataba wa udhamini kati yake na Kilimo Sports Club kwa kipindi cha miaka mitatu. Katika hafla hiyo Savoy Farm Ltd iliwakilishwa na Bwana Omary Issa, ambaye pia aliwakabidhi Kilimo Sports Club dazani moja ya jezi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkataba huo.Wakati huo huo timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika leo inatarajiwa kupimana nguvu na timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani saa 8.45 mchana katika Viwanja vya Magereza Ukonga.

Tuesday, September 9, 2014

Benki na Mfumo Mpya wa Pemebejeo za Kilimo
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Christopher Chiza leo amekutana na wamiliki wa benki mbalimbali lengo likiwa ni kujadili namna watakavyo imarisha mfumo mpya wa utoaji wa pembejeo za ruzuku kwa njia ya mikopo.
Akiongea mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa taasisi ya Bodi ya sukari amewataka wamiliki wa benki hizo kuwekeza katika mazao ya chakula kama mpunga na mahindi badala ya mazao ya  biashara pekee.
Aidha amezitaka taasisi hizo za fedha   kutumia mitandao yao ili kuwafikia wakulima wengi zaidi, maeneo ambayo taasisi hizo hazitaweza kuyafikia  kilimo cha mkataba kitumike kukamilisha dhana hiyo.

Monday, September 8, 2014

Kikao cha Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki chafanyika Kigali nchini RwandaMhe. Eng. Christopher K. Chiza (Mb) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, akitia  saini katika  Taarifa ya Kikao cha Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula  wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kikao kilifanyika Kigali nchini Rwanda hivi karibuni.

 
 Mhe. Eng. Christopher K. Chiza (Mb) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Akitia saini katika kitabu cha wageni baada ya kutembelea Makumbusho ya Mauaji ya Kimbali yaliyofanyika nchini Rwanda

Mhe. Eng Christopher K. Chiza (Mb) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika na Mhe. Dr. Kebwe StepheneKebwe (Mb) Kwa pamoja wakiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la pamoja walilozikwa  wahanga wa mauaji ya Kimbali nchini Rwanda.
Mhe. Eng Christopher K. Chiza (Mb) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika na Mhe. Dr. Kebwe Stephen Kebwe (Mb) wakisali kwenye  Kaburi la pamoja walilozikwa  wahanga wa mauaji ya Kimbali nchini Rwanda baada ya kuweka Shada la maua.


Friday, September 5, 2014

Mhe. Chiza kuhudhuria mkutano wa Usalama wa Chakula


Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Eng. Christopher Chiza  leo amehudhuria mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afrika Mashariki  unaofanyika Kigali nchini Rwanda.
Aidha mkutano huo wa siku moja mawaziri hao watakuwa wanajadili hali ya usalama wa Chakula barani Afrika