Sunday, December 28, 2014

Mhe. Christopher K. Chiza (Mb) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, akifanya mazungumzo na mwenyeji wake, Mhe. Cao Duc Phat Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijijini wa Jamhuri ya Kishoshalisti ya Vietnam

ZIARA YA MHE. CHRISTOPHER K. CHIZA (MB) KATIKA NCHI YA JAMHURI YA KISOSHALISTI YA VIETNAM

Mwezi Desemba 2014, Mhe. Christopher K. Chiza (Mb) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, alifanya ziara ya siku tano, katika nchi ya Jamhuri ya Kishoshalisti ya Vietnam. Ziara hiyo ilikuwa ni utekelezaji wa Maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Kishoshalisti ya Vietnam, ya kuwa na mazungumzo ya pamoja kwa ajili ya kuunda Tume ya pamoja ya kuendeleza kilimo katika nchi hizi mbili.
Mazungumzo yaliyofanyika yalihusu hatua ya kutia saini Mihtasari (Minutes) zitakazopelekea kufikia utiaji saini wa makubaliano yatakayofikiwa ya kuanzisha Tume ya pamoja ya Kilimo. Utiaji wa saini wa makubaliano hayo unategemea kufanyika  mwezi Julai 2015 nchini Tanzania
Mhe. Christopher K. Chiza (Mb) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika na Mhe.Cao Duc Phat Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijijini wa Jamhuri ya Kishoshalisti ya Vietnam wakitia saini Mihtasari (Minutes) ya makubaliano kuelekea kuunda Tume ya pamoa ya Kilimo
Mhe. Christopher K. Chiza (Mb) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazunguzo ya pande mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kishoshalisti ya Vietnam