Friday, February 27, 2015

Jukwaa la kujenga uwezo wachambuzi wa Sera katika Sekta ya Kilimo lazinduliwa.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Dkt. Yamungu Kayandabila (kulia) akibabidhiwa vifaa vya mawasiliano na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bwana, Harold Carey katika ukumbi wa mikutano, Makao ya Wizara, (kushoto) ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bi. Janeth Simkanga.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Dkt. Yamungu Kayandabila akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi ya Jukwaa la kuboresha uchambuzi wa Sera katika Sekta ya Kilimo, Makao Makuu ya Wizara.

Mratibu wa Mradi wa Maendeleo unaojikita katika kuboresha Uelewa katika Masuala ya Sera, katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Bwana Joseph Karugia akifafanua jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Mradi wa Kuwajengea uwezo Wachambuzi wa Sera katika Sekta ya Kilimo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Jana.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Dkt. Yamungu Kayandabila leo amezindua rasmi Jukwaa la kujenga uwezo wachambuzi wa Kuratibu masuala ya Sera kwenye Sekta ya Kilimo, mradi unaojulikana kama (PAPAC- Platform for Agriculture Policy Analysis and Coordination).
Jukwaa hilo lina mchanganyiko wa wataalam kutoka Wizara za Sekta ya Kilimo, Taasisi zinazojihusisha na masualaya kilimo, pamoja na Sekta Binafsi, wataalam hao ni kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda na Biashara na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Wataalam wengine ni kutoka, Mpango wa Maendeleo ya Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania SAGCOT, Ofisi ya Rais inayoratibu Maendeleo ya Sekta ya Kilimo, PDB na Shirika lisilo la Kiserikali lenye kujihusisha na Kilimo, ANSAF.
Akizindua Jukwaa hilo, Naibu Katibu Mkuu alisema, Serikali ya Tanzania imedhamiria kuleta mapinduzi ya kweli katika kilimo na kuongeza kuwa, uzinduzi wa Jukwaa hilo, ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Sekta ya Kilimo Afrika, CAADP.
Aliongeza kuwa Jukwaa limeundwa lengo likiwa ni kutoa kipaumbele kwenye kuboresha Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo, ASDP II ambapo chini ya Mpango huo msisitizo umewekwa kwenye kuboresha masuala ya sera.
Sambamba na uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu pia alipokea vifaa vya mawasilino vyenye thamani ya Shilingi Milioni 160, lengo likiwa ni kuboresha  mawasilino kwa ajili ya kuwawezesha wataalam wa sera walio katika Wizara za Sekta ya Kilimo kurahisisha utendaji wao wa kazi.
Vifaa hivyo ni pamoja na kompyuta za viganjani, ‘palmtop’ aina ya Samsung Tab 4, na simu za mkononi aina ya Samsung Note 4, kifaa cha video ya mawasiliano yenye uwezo wa kuwasilina na mtu mmoja au mkutano kwa wakati mmoja.
Vifaa vingine ni pamoja na Kopyuta za mezani aina ya Toshiba, na vifaa vingine vya kiofisi kama makabati ya kisasa na meza.
Naibu Katibu Mkuu aliongeza kuwa vifaa hivi vitasaidia katika kuwakutanisha pamoja wadau wote wa maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kuleta maboresho ya sera.
Dkt. Kayandabira aliwashukuru Wabia wa Maendeleo, kwa kufanikisha uanzishwaji na utekelezaji wa Jukwaa hili. Wabia hao wa Maendeleo ni pamoja na Shirika la Misaada la Marekani, USAID, Chuo Kikuu cha Michigani na Mradi wa Maendeleo wenye Kuboresha Uelewa katika masuala ya Sera, Mradi huo unajulikana kama (ReSAKSS- Regional Strategic Analysis and Knowledge Support System). Mpango unaotekelezwa katika Kanda ya Afrika ya Kati na Mashariki.

Wednesday, February 18, 2015

Ziara ya Mheshimiwa Wasira nchini ItaliaWaziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa  Stephen Wasira akihutubia mkutano wa 38 wa IFAD uliofanyika hivi karibuni jijini Rome nchini Italia.

Monday, February 16, 2015

Kwaheri njaa kwaheri, karibu soko mazaoHongereni wakulima, mahindi mmezalisha
Mmezalisha kwa tija, njaa hadi kukomesha
Ni mahindi na mtama, mpunga mkaboresha
Kwaheri  njaa kwaheri, karibu  soko mazao

Wizara ikajipanga, miundombinu imarika
Si Moro wala si Manga, maji yakafurika
Mpanga lupiro Ulanga, huko tija ikaongezeka
Kwaheri  njaa kwaheri, karibu  soko mazao

Maswali yakaulizwa, soko letu liko wapi
Tuwauzie wazawa au  wakina mukingiki
Hifadhi ya chakula, mbona hamtufikii
Kwaheri  njaa kwaheri, karibu  soko mazao

Zalisheni kwa ubora, soko litaongezaka
Zao bora ni  kombora, hadi nje linaruka
Jiungeni na ushirika, maghala yameimarika
Kwaheri  njaa kwaheri, karibu  soko mazao

Lima kwa kulenga soko, serikali si mnunuzi
Nahifadhi tu ya kesho, wakuliama wote siwezi
Imarisha vifungashio, kauzeni hadi uswazi
Kwaheri  njaa kwaheri, karibu  soko mazao


Na BASHIRI SALUM MSANGI