Tuesday, May 12, 2015

Nafasi za kujiunga vyuo vya kilimo.

Nafasi za kujiunga vyuo vya kilimo. Tembelea na Omba kujiunga hapa.
http://www.kilimo.go.tz/Organization%20structure/Training/training%20institutions.html

Friday, May 8, 2015

Mhe. Stephen Wassira amepokea msaada wa mbolea


 Mheshimiwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirirka Stephen Wasira (katikati) akiwa na Balozi wa Japan Bwana Masaharu Yoshida (kulia) na mwakilishi wa Shirirka la Maendeleo la Japan (JICA) Nagase Toshio katika hafla hiyo

 Mheshimiwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirirka Stephen Wasira, akimkaribisha Balozi wa Japan Bwana Masaharu Yoshida

Sehemu ya mbolea iliyokabidhiwa kwa Wziri wa Kilimo Chakula na Ushirika na Balozi wa Japan


Mheshimiwa Waziri katika picha ya pamoja


Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Stephen Wassira amepokea msaadsa wa mbolea aina ya Urea kiasi cha tani 7,492.7 kutoka Serikali ya Japan. Mbolea hiyo inarhamani ya Yen I Milioni 380 sawa na Shilingi Bilioni 5.7 chini ya mpango wa ushirikiano kati ya  Tanzania na Japan, unaojulikana kwa jina LA KR II 2013.
 Akipokea Mbolea hiyo, Mhe. Wassira aliishukuru Serikali ya Japan kupitia Barozi wake, Masaharu Yoshida ambaye alimkabidhi sehemu ya shehena hiyo ya Mbolea katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara, Barbara ya Mandera, Jijini Dar es Salaam.

Mhe.Wassira alisema msaada huo wa mbolea umekuja wakati sahihi kwani katika maeneo mengi ya nchi ni wakati wa  mavuno na kwamba utarahisisha uzalishaji wenye tija katika msimu ujao wa kilimo ambao utaanza mara baada ya kipindi cha mavuno kumalizika.
Waziri Wassira aliongeza kuwa, shehena hiyo ya mbolea itapelekwa kwa wakulima wadogo ambao ndiyo waliowengi katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula kama vile Nyanda za Juu kusini, lengo la Serikali ni kuongeza tija katika uzalishaji endelevu.
Naye Balozi wa Japan nchi, Bwana Masahau Yoshida alisema msaada huo wa mbolea ambao Serikali ya Japan imetoa kwa Tanzania unalenga kwa makusudi kubadilisha maisha ya wakulima wadogo kwa lengo la kuongeza tija kwenye kilimo na kwamba ni furaha ya Serikali ya Japan kuwasaidia wenzao wa Tanzania.
Serikali ya Japan na Tanzania chini ya Mpango wa KR I na KR II zilianza kutekeleza Mpango huo tangu mwaka 1978, katika utekelezaji wake,  Tanzania  imekuwa ikinufaika katika maeneo mbalimbali si kwa Sekta ya Kilimo lakini pia Sekta ya Afya na Nishati, kwa kipindi cha miaka 36 iliyopita jumla ya shilingi bilioni 31.5 zilitolewa na Serikali ya Japan ili kugharamia miradi 200 ambayo, ilitekelezwa chini ya Mpango huo.