Thursday, June 11, 2015

Plant Breeder's Rights meetings

From Left: Dr. Hussein Mansoor, Assistant Director, Crop Development; Mr. Geoffrey Kirenga, CEO SAGCOT; Mr. Canut Komba, Assistant Director Agricultural Inputs, Mr. Patrick Ngwediagi, Registra of Plant Breeder's Rights; and Mr. Bob Shuma, CEO TASTA.
 


Dr. Fidelis Myaka Afungua Mkutano wa Wadau wa MbeguDr. Fidelis Myaka Afungua Mkutano wa Wadau wa Mbegu


katika hotuba ya ufunguzi, Dr. Myaka alianza kwa kuwashukuru Washiriki wote wa Mkutano. Vilevile  alisisitiza kuwa Mbegu Bora ni pembejeo muhimu katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo hapa nchini. Kwa maana hiyo bila mbegu bora nchi haiwezi kuwa na chakula cha kutosha na hivyo  kuhatarisha usalama wa Taifa. 

Dr. Myaka alieleza kuwa nchi bado ina changamoto nyingi mojawapo ni kutojitosheleza mahitaji yake ya mbegu. Hivyo, alieleza kuwa ni azma ya Serikali  kuona kuwa uzalishaji  na upatikanaji wa mbegu hapa nchini unaongezeka. Serikali pekee yake haitaweza kufanikisha azma hiyo, bali inatakiwa kushirikiana na wadau wote wa mbegu kuzalisha mbegu za kutosha. 

Mgeni rasmi aliwaeleza washiriki kuwa, mkutano wa leo ni muhimu sana kwa wadau kuelewa mambo muhimu ili kufikia malengo yaliyokusudia. Aliwataka wadau kuchangia mawazo ili kuboresha maeneo yanayoleta ukakasi katika kuboresha tasinia ya mbegu hapa nchini. 

Suala jingine muhimu la kufanyia kazi ni kuhakikisha mbegu zilizotolewa na watafiti na kuruhusiwa kutumika kwa miaka mingi zinawafikia wakulima. 

Suala jingine la kuzingatia ni kuhakikisha kuwa sekta binafsi inapata mbegu za umma ili  ziweze kuzalishwa kwa wingi. Aidha, ubora wa mbegu zinazozalishwa lazima uzingatiwe kufikia viwango vya kimataifa. 

Malengo yote hayo yatafikiwa tu ikiwa kila mdau atakaa katika nafasi yake na hivyo sote kwa pamoja tuweke mikakati ya kufikia maendeleo ya kilimo hapa nchini. 

Mgeni rasmi alimaliza kwa kuwashukuru washirika wa maendeleo hususan AGRA na USAID kwa kusaidia rasilimali za kufanikisha mkutano huo. Aidha, aliwashukuru wadau kwa kushiriki katika mkutano.

 
image1.JPG