Thursday, September 10, 2015

SERIKALI  NA WADAU WA MBOLEA WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO 

Mchumi Mkuu  Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika  Bi. Magreth Ndaba amesema Serikali inajitahidi kuwezesha mbolea kupatikana kwa wakati na kwa bei nafuu ingawa badozipo changamoto zinazozuia  matumizi ya Mbolea kwa wakulima. Bi. Margreth ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa mbolea uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Aidha, Mratibu wa Mradi wa MIRA Ndg; Gungu Mibavu alisema dhamira ya mkutano huu ni kupata maoni kutoka kwa wadau juu ya nini kifanyike katika kurahisisha biashara na usambazaji wa mbolea kwa mkulima. Mkutano huo ulijumuisha  wadau  kutoka Vyuo vikuu,Sekta binafsi, na taasisi za Serikali kama Wizara ya Kilimo Chakula na Ushika, TRA na TFRA. Mkutano huo umelenga yafanyike mabadiliko ya  kisera yatayowezesha upatikananji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu na hivyo mkomboa Mkulima.
Kwa upande wa sekta binafsi Dokta Endrew Msolla amesema anaamini kitakachojadiliwa katika mkutano huo  kitasikilizwa na Serikali na kutekelezwa kwa haraka ili mkulima anufaike na mbolea.  Hata hivyo alisema kuwa mkulima anapitia changamoto tatu ambazo ni pamoja na gharama ya mbolea,Mbolea kutofika kwa wakati,  uelewa mdogo wa matumizi ya mbolea, ambayo yote haya yatajadiliwa na wadau katika mkutano.