Monday, October 5, 2015
TANZIA

 
 Marehemu Dkt. Amandus Lwena
 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi mwenzao marehemu Dkt. Amandus David Lwena kilichotokea siku ya Ijumaa tarehe 02/10/2015 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Jijini, Dar es salaam.
 
Marehemu Amandus David Lwena alizaliwa tarehe 19/9/1962 katika hospitali ya Njombe. Mwaka 1973 - 1979 alimaaliza elimu  yake ya msingi katika shule ya Msingi, Kingole Mkoani Mbeya. Mwaka 1980-1983 alihitimu elimu ya sekondari, kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Tosamaganga  iliyopo Mkoani Iringa. Mwaka 1984 - 1986 alihitimu elimu ya kidato cha sita katika shule ya sekondari  Azania Mkoani  Dar es salaam. Mwaka 1987-1991 alihitimu Shahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Kilimo katika chuo Kikuu cha kilimo Sokoine Sokoine (SUA).

Mwaka 2007- 2008 alihitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Washington nchini Marekani na mwaka 2008 - 2010 alihitimu  Shahada ya Uzamivu katika Masuala ya mipango ya rasilimali maji na maendeleo ya umwagiliaji.
Marehemu Amandus David Lwena alianza kazi mwaka 1991 katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (ARI) KATRIN mwaka 1994 aliamia Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika katika Idara ya Umwagiliaji na Huduma za Ufundi ambapo alifanya kazi katika nafasi mbalimbali mpaka umauti unamkuta, marehemu Amandus ­­­­­­­­­­­­David Lwema alikuwa Mkurugenzi Msaidizi  wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. 

Taifa limepoteza mtumishi aliyekuwa mchapakazi na aliyefanya kazi kwa uweredi katika kipindi cha uhai wake.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE AMINA.