Monday, January 18, 2016WIZARA YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWATUMIA WAHITIMU WA VYUO VYA KILIMO WALIOSOMA KOZI MAALUM

Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi inautangazaia umma kuwa wahitimu mahiri 10,629 waliofuzu Vyuo vya Kilimo vya Inyala, Mtwara, Horti Tengeru, Igurusi, Katrin, Ukiriguru, Maruku, Uyole, KTC Moshi, Mlingano, Tumbi, Ilonga, NSI Kidatu  na Mubondo, wanaweza wakatumiwa kwa lengo la kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo.
Jumla ya wahitimu 7,525 wamefaulu katika ngazi ya Astashaada kati ya hao, wanawake ni 2,557 na wanaume ni 4,968. Wahitimu 3,104 wameafaulu katika ngazi  ya Stashahada (Diploma) ambapo  wanawake ni 774 na wanaume 2,370.
Wahitimu hawa ni mahiri katika michepuo ya Stashahada ya fani ya kilimo cha mboga matunda na maua (Horticultural Crops), Zana za Kilimo, Uzalishaji wa Mazao, Umwagiliaji na Huduma za Kiufundi, Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo na Chakula na Lishe.
Aidha, Wahitimu hao wanauwezo wa kiutendaji katika kuanzisha na kutunza bustani za mimea, mboga na matunda, kushauri wakulima kwa kutumia teknolojia mbalimbali ikiwemo TEHAMA, kusimamia kazi zote zinazohusu matumizi ya Zana za Kilimo na kuzifanyia matengenezo kila itapohitajika, kujenga miundombinu ya shamba ikiwemo maghala, vihenge na mabanda ya wanyama mbalimbali.
Pia wanauwezo wa kuzalisha mazao makuu ya chakula na biashara yanayolimwa nchini, kusaidia tafiti na kukusanya takwimu za utafiti wa mazao, kusimamia ujenzi wa miradi midogo ya umwagiliaji na kuandaa michoro ya miradi hiyo.
Wahitimu hao pia wanao uwezo wa kuandaa mazao baada ya kuvunwa, kuchakata na kufungasha, kufanya tathmini ya lishe na mahitaji ya chakula katika jamii, kuandaa mipango na kutoa ushauri kwa jamii kuhusu masuala ya lishe.
Serikali inawafahamisha Wadau wa maendeleo ya kilimo na mifugo, Wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi na yeyote mwenye mahitaji yanayoweza kutekelezwa na wataalam hawa kuwa wanayo fursa ya kuwaajiri, wahitimu hao ili kupata ufanisi katika shughuli zao za kilimo.

Imetolewa na;
                                  
                    Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI
                                           18/01/2016

Wednesday, January 13, 2016

waziri. Nchemba akutana na Balozi wa Beligium kujadili fursa ya kilimo katika zao la muhogo
Waziri Nchemba atoa wito kwa wakulima wa mihogo kuchangamkia fursa ya kuzalisha zao hilo kwani soko lipo ndani na je ya nchi

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba alitoa wito huo kwa Wakulima waktia wa mazungumzo ya kikazi na Balozi wa Ubeligiji nchini Mheshimiwa Paul Cartier wakati alipomtembelea ili kujitambulisha na kumpongeza.

Waziri Nchemba alisema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na mkazo umewekwa kuongeza uzalishaji na uongezaji wa thamani mazao ya kilimo.

Waziri Nchemba alimwambia Balozi Cartier kuwa Serikali imedhamiria kubadilisha hali ya uchumi ya Watanzania wa kipato cha chini na cha kati na kwa maana hiyo mkazo ni kuongeza uzalishaji ambao kwa kipindi kirefu umekuwa ndiyo tatizo.

Waziri Nchemba amesema kwenye suala la ubora kwa zao hilo si tatizo kwani Serikali kupitia Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi imejenga mahabara ya kisasa kwa ajili ya kuzalisha vipando bora na kwamba watafiti katika Kanda ambazo mihogo imekuwa ikizalishwa, wamekuwa wakizalisha vipando bora na vya kutosha kwa ajili ya kutosheleza wakulima wengi. 

Waziri Nchema alimuakikishia Balozi huyo kuwa Mikoa ya Pwani, Kanda ya Ziwa na Ukanda wa Ziwa Tanganyika uzalishaji utaongezeka mara dufu kwamba ni nafasi ya Wakulima kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo kwa wingi kwani soko lipo na uhakika.

Awali Bibi Margareth Ndaba Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Kimataifa, Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi alimueleza Waziri Nchemba kuwa Tanzania imepokea maombi ya kuuza mihogo yake nchini China na kuongeza kuwa ni fursa kwa Wakulima wa Tanzania kuichanghamkia fursa hiyo kwani kiwango kinachotakiwa ni kikubwa ukilinganisha na uzalishaji


Monday, January 4, 2016

Makatibu Wakuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wafika rasmi katika ofisi zao tayari kuanza kazi

Katibu Mkuu Kilimo, Dkt. Florence Turuka, Katibu Mkuu Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba na Katibu Mkuu Mifugo, Dkt Maria Mashingo leo wamefika katika ofisi zao tayari kuanza kazi ya kuwatumikia Watanzania.

Katibu Mkuu Kilimo, Dkt. Florence Turuka alifika katika ofisi yake Kilimo I na kupokewa na Wakuu wa Idara na Vitengo wakiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Utawala Bibi Mary Temba aliyemtambulisha Katibu Mkuu kwa Watumishi kadhaa waliofika kumpokea.

Mara baada ya mapokezi hayo, kwa pamoja Dkt. Florence Turuka, Dkt Maria Mashingo na Dkt. Yohana Budeba walikuwa na mazungumzo na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ambaye aliwaomba kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kuwatumikia Wananchi wa Tanzania ambao wengi wao ni Wakulima na Wafugaji.

Mara baada ya mazungumzo mafupi na Waziri, Katibu Mkuu Kilimo, Dkt. Florence Turuka alikutana na Wakuu wa Idara na Vitengo kwa lengo la kufahamiana, aliwashukuru kwa mapokezi waliyompa na kuwaomba kuwatumikia wananchi ambao wana matumaini makubwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

“Nawashuru sana kwa mapokezi mliyonipa, niwaombe tufanye kazi kwa bidii na maarifa ili kuongeza tija na ufanisi kwa kuwa tunawajibu wa kutumiza ahadi za Mheshimiwa Rais alizoahidi wakati wa uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge mwezi Oktoba, 2015.” Alikaririwa Dkt. Turuka.