Thursday, February 25, 2016

MBUZI WALIOPO KATIKA SOKO LA VINGUNGUTI LISILO RASMI WATAKIWA WAONDOLEWE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo naUvuvi Dokta Maria Mashingo amewataka wadau wa soko na machinjio ya mbuzi katika eneo la Vingunguti kuondoka katika eneo hilo ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya serikali unaofanywa na wachinjaji wanao kwepa kushusha mifugo yao katika mnada wa pugu kwa kutokuwa na vibali vya maeneo watokako na kulisababisha ukosefu wa  mapato kwa Serikali.
Katibu Mkuu aliyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo katika eneo la Vingunguti na kuzungumza na wafanya biashara na wachinjaji wa mbuzi   na kuwambia kuwa kiutaratibu eneo linatakiwa kufutwa kabisa  kwa kuwa siyo rasmi kwa machinjio ya mbuzi.
Aidha akizungumzia sheria  ya magonjwa  ya mifugo namba 17 , Mkurugezi wahuduma za afya ya mifugo Dokta Abdi Hyagaimo alisema kuwa, “wanyama wote wanaotoka katika mnada wa awali waletwe katika mnada wa Upili ambao ni Pugu sasa hapa katika eneo la Vingunguti wanafanya nini” aliuliza Dokta Abdi.
Nao wafanyabiashara kwa nyakati tofauti walitoa moni yao kwa Katibu Mkuu huyo kuwa eneo hili limeanza kutumika kwa muda mrefu hivyo ni vizuri wakaachiwa waendelee na biashara ya mbuzi na machinjio kwa kuwa wamelizoea na ndiyo tegemeo kwa maisha yao .
Bwana Yasini Shabani  mfanya biashara wa mbuzi katika eneo la Vingunguti alisema kuwa tangu enzi za wazee wetu walikuwa wanafanya biashara hapa. Hivyo tunaomba tuboreshewe eneo hili liwe rasmi kwa biashara ya mbuzi na machinjio.
Hata hivyo siyo Vingunguti pekee ambalo ndiyo  soko lisilo rasmi la mbuzi, kuna masoko ya namna hiyo katika jiji hili  yanayofanya shughuli hii ya kuuza na kuchinja mbuzi.
Mdau wa biashara ya mbuzi katika eneo la Vingunguti bwn Amri Hamis aiyataja maeneo mengine kuwa ni Jangwani ,Tegeta , Mbezi na Kariakoo.
Hata hivyo Doktari wa Mifugo katika mnada wa Vingunguti  bwn Reuben Nyaisa alimweleza Katbu Mkuu huyo   kuwa mapato yameongezeka kuanzia kipindi cha tangu Disemba hadi Januari kwa kuimarisha usimamizi madhubuti katika vituo vya kupokea kushushia na manjinjioni. Hivyo kuanzia  Disemba, 2015 hadi Januari 2016 mapato yameongezeka na kufikia wastani wa million 35 kwa mwezi alisena Dokta Nyaisa. 
Serikali ya awamu ya tano inasisitiza udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali ili kuhakikisha mapato yanapatikana kwa kila eneo ambapo ushuru unatakiwa kulipwa.Tuesday, February 16, 2016

MRADI WA STARS UTASAIDIA KUBORESHA KILIMO NCHINI.


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Dr. Yohana Budeba, amewaasa watafiti nchini kuhakikisha kuwa, matokeo ya utafiti yanawafikia walengwa hasa wakulima wadogo.
Hayo ameyasema wakati anafungua warsha ya wadau katika Mradi wa STARS iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar Es Salaam. “Ni muhimu taarifa sahihi kutoka kwa watafiti ziwafikie wakulima haraka kwa wakati zinapohitajika”alisema Dr. Budeba.
Utafiti unaofanywa na Mradi wa STARS unalenga kutumia technolojia ya utambuzi kwa njia ya satelaiti na ndege zisizo na Rubani ili kuboresha shughuli za kilimo katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia kusini.
Taarifa zinazokusanywa kwa njia hii zinaweza kutolewa ushauri kwa wakulima mashambani kusaidia kufanya maamuzi yao kuhusu mbinu za kilimo. Hii inasaidia upatikanaji wa mazao bora na uzalishaji endelevu. Pia zinaweza kusaidia katika maamuzi ya ngazi ya juu serikalini katika kusimamia usambazaji wa chakula kitaifa wakati wa ukame kwa usahihi zaidi.
Afrika Mashariki mradi huu unatekelezwa Tanzania na Uganda ambao unafanya ufuatiliaji wa hatua za ukuaji wa mazao kuanzia kupanda hadi kuvuna katika mashamba tofauti tofauti ya mazao ya chakula ili kupeleka taarifa kwenye Idara ya Usalama wa Chakula na kusaidia kufuatilia hali ya mazao.
Faida kubwa ya mradi wa STARS ni utabiri wa mavuno katika ngazi ya kitaifa ili kufanya maamuzi ya hali ya chakula nchini vile vile inategemewa kuwa, masoko ya ndani yataimarika wakulima wakizalisha kwa ufanisi na kuwa na fursa nzuri ya kuuza mazao nje ya nchi.
Mradi huu unafadhiriwa na Bill & Belinda gates Foundation, na ulianza rasmi julai 2014 na kufikia ukomo wake Juni 2016. Washiriki katika mradi huu ni Wizara ya kilimo Mifugo na Uvuvi, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, na Chuo kikuu cha Marland cha Marekani.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa mkutano wa Mradi wa STARS
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Dr.Yohana Budabe (upande wa kulia) wakijadili jambo na wajumbe wa mkutano


Sunday, February 7, 2016

wachakataji wa dagaa waliofanikiwa kutokana na mafunzo ya mradi wa kuendeleza kilimo na Uvuvi TASP II

Mradi wa Uboreshaji wa Kilimo na Uvuvi waonyesha Mafanikio makubwa kwa wavuvi wa Mikoa ya kanda ya ziwa victoria

 vijana walioajiriwa kuchakata dagaa  wakiwa kazini


Mradi wa Uboreshaji wa Kilimo na Uvuvi waonyesha Mafanikio makubwa kwa wavuvi wa Mikoa ya kanda ya ziwa victoria

Wavuvi wadogowadogo wa kanda ya ziwa wamefaidika na Mradi wa uboreshaji wa huduma za kilimo na uvuvi  TASP II kwa kufungua na kuendeleza masoko ya bidhaa hizo.
Hayo yamebainika baada ya ziara iliyofanywa na  wanahabari wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi katika mikoa ya Kagera,Mwanza na Mara uliofanyika hivi karibuni.
Wakiongea na baadhi ya wajasiriamali hao wilayani muleba wamesema mradi huo umewasaidia katika mabadiliko ya uandaaji na uboreshaji wa soko la dagaa.


 mafunzo yaliyotolewa kwa wanavijiji kuhusu uchakataji wa dagaa kuliongeza ari ya uwajibikaji


vijana wanaojishughulisha na uchakataji wa dagaa baada ya kukutana na wanahabari kutoka wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi hivi karibuni

Monday, February 1, 2016

Watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WKMU Wafanya kikao cha kazi
Watumishi wa Kitengo cha Mawasilinao ya Serikali cha Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi leo wamefanya kikao cha pamoja wa kazi tangu Wizara hiyo iundwe na kuwa Wizara moja.
      Itakumbukwa kuwa Mwezi Desemba, 2015 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, aliunda Baraza Jipya la Mawaziri na kuunda Wizara mpya kwa kuziunganisha baadhi ya Wizara. Aidha Iliyokuwa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi iliunganishwa na kuwa Wizara moja ambayo inafahamika kama Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.
      Akifungua mkutano huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Mifugo na Uvuvi) Bibi Judith aliwambia Wajumbe waliohudhuria kuwa kikao hicho kilikuwa kinalenga  kuboresha utendaji kazi wa Kitengo cha Mawasiliano katika mtazamo mpya baada ya kuunganishwa Wizara mbili.
Katika kikao hicho Wajumbe walipata fursa ya kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati mipya na namna ya kuboresha utendaji wao wa kazi za kila siku.
      Aidha, Watumishi walitoa maoni na kupendekeza muundo mpya wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ambapo msisitizo ulikuwa ni kuboresha katika utoaji wa taarifa kwa Umma, kuisemea Serikali, kushughulikia malalamiko ya Watumishi, Wadau na kuunda Dawati la msaada wa taarifa kwa wananchi na wadau wa Sekta ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.
      Mapendekezo mengine yalikuwa ni kuunda Sehemu ndogo ndani ya Kitengo ili kuimarisha utendaji wa kazi za kila siku za Kitengo
      Sehemu zilizopendekezwa ni pamoja na  Sehemu itakayoshughulikia Mawasiliano ya Kielektroniki yaani Redio na Televisheni, Sehemu ya Mawasiliano kwenye Machapisho na Sehemu ya Mawasiliano itayojihusisha na Mahusiano na Matangazo.
      Mapendekezo mengine ni kuwa na Sehemu ya Huduma za Maktaba na Mawasiliano ya Mitandao ya Kijamii.
      Kikao hicho kimefanyika siku moja kabla ya kufanyika kwa mkutano wa pamoja siku ya Jumanne tarehe 2 Februari, 2016 katika Ukumbi wa Media Centre uwanja wa Taifa ambao umeitishwa na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora. Lengo likiwa ni kuunda Muundo Mpya wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.

watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wamekutana katika ukumbi wa kitengo hicho na kujadili namna ya kuboresha utendaji kazi katika sekta hizo.


 Maafisa wa Mawasiliano wakipitia habari magazetini leo katika moja ya kumbi za mikutano iliyopo katika jengo la Mvuvi House