Monday, May 30, 2016

MBEGU MPYA ZA MAZAO MBALIMBALI ZAIDHINISHWA                    
Kamati ya Taifa ya Mbegu (National Seed Committee) imeidhinisha matumizi ya aina 29 za mbegu mpya za mazao mbalimbali ya kilimo, mazao hayo ni mahindi,mpuga,alizeti karanga na chai.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Nchemba kwa vyombo vya habari, inasema kuidhinishwa kwa aina hizo za mbegu kunafuatiwa mapendekezo yaliyofanywa na kamati ya Taifa ya kupitisha aina mpya ya mbegu za mazao (The National variety Release Committee) katika kikao kilichofanyika kuanzia tarehe 16 – 17 Machi 2016, makao makuu ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Jijini Dar es salaam.
Aidha, aina hizo mpya za mbegu zimefanyiwa utafiti na kugundulika kuwa zinasifa mbalimbali ikiwemo kustahimili ukame,kutoa mavuno mengi,ukinzani dhidi ya magonjwa na wadudu,kukomaa mapema na kupendwa na wakulima.
Mhe. Nchemba aliongeza kuwa utafiti wa kina ilifanjwa na vyuo za kitafiti visivyopungua 12 apa nchini na kuweza kuzalisha aina mpya za mbegu ivyo kupatikana aina 16 za mahindi,2 za mpunga, 4 za alizeti, 3 za karanga na 4 za chai.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa aina hizo za mbegu zitaanza kuzalishwa na makampuni mbalimbali ya uzalishaji mbegu pamoja na Wakala wa Taifa wa mbegu za kilimo (Agriculture Seeds Agency-ASA),  kwa lengo la kuzifikisha aina hizo mpya za mbegu bora  kwa wakulima kuanzia msimu ujao wa kilimo 2017/2018.
“ Hatua hiyo ya kamati inalenga kuongeza tija na kipato kwa mkulima”, iliongeza sehemu ya taarifa hiyo ya Mhe. Nchemba.Monday, May 23, 2016

INDIA YAVUTIWA NA JITIHADA ZA TANZANIA KUINUA KILIMO

Seriakali ya India imevutiwa na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake za kuboresha kilimo hapa nchini.
Hayo yalisemwa na Balozi wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya alipotembelea Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi na kuzungumza na jopo la viongozi wa juu wa wizara hii.
Bwana Arya alieleza kuwa nchi ya India ina uzoefu mkubwa katika sekta ya kilimo katika nyanja mbalimbali ikiwemo uboreshaji na uzalishaji wa mbegu, huduma za ugani, pembejeo za kilimo zikiwemo mbolea na madawa mbalimbali ya kupambana na magonjwa na wadudu yanayoathiri mazao.
Pia alielezea ushirikiano uliopo wa uuzaji wa zana za kilimo ikiwemo matrekta na zana nyingine za kilimo kupitia SUMA JKT.
Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo hayo ulianisha mambo mbalimbali ambayo Tanzania na India zinaweza kushirikiana katika jitihada za kuinua kilimo.
Mkurugenzi wa Zana za Kilimo Eng. Mark Lyimo, kwaza aliishukuru Serikali ya India kwa jitihada zake za kuendeleza kilimo kwa wakulima wa Tanzania na hasa kwa kusaidia upande wa zana za kilimo.
Eng. Lyimo alimkumbusha Bwana Arya ahadi ya serikali yake ambayo ilitolewa na India wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne ya kutaka kusaidia kufadhili miradi mbalimbali ya kuendeleza kilimo.
“India ione uwezekano wa kutoa mafunzo kwa watalaamu wa Tanzania ili kuboresha matumizi sahihi ya zana za kilimo ili kuleta ufanisi” aliongeza Eng. Lyimo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo Dkt. Hussein Mansoor aliiomba India kusaidia kilimo cha mazao ya biashara na pia kubadilishana uzoefu katika kilimo kwa kutumia uzoefu wa India.

Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Uratibu wa Misaada ya Kimataifa ya Maendeleo ya Kilimo Bi. Margareth Ndaba kwa niaba ya Katibu Mkuu.

Wajumbe wa Tanzania na India wakiwa katika mazungumzo

Bi.Margareth Ndaba akipata maelezo kutoka kwa balozi wa India Bw.Arya


Thursday, May 19, 2016

TURUKA : MWONGONZO WA KUKABILIANA NA TABIANCHI UTALETA MAFANIKIO
Wataamu wa kilimo wamekutana na wadau wengine kupitia Mwongozo wa kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi ili kuongeza uzalishaji wa mazao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi  Dkt. Florence Turuka amesema  Mwongozo huo utasaidia kuleta teknolojia mbali mbali ya mazao yanayoendana na hali ya sasa ya mabadiliko ya tabianchi .
Mwongozo huo utasaidia kuwaelimisha wadau wa sekta ya kilimo  ili kupambana na mabadiliko yanayoletwa na mbadiliko ya hali ya hewa kwa sasa.
Dkt. Turuka amefahamisha kuwa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) wamesaidia  kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na hali hii.
Kwa mujibu wa Dkt. Turuka,  badhi ya athari zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa Sekta ya Kilimo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa joto, mlipuko wa magonjwa na wadudu katika kilimo, kuwepo kwa tabia ya mazao kuhitaji maji mengi, mafuriko na ukame.
’Watalaamu katika warsha wataibuka na mapendekezo mazuri yatakayosaidia kuboresha mwongozo huu katika kuinua kilimo’ aliongeza Dkt. Turuka katika hotuba yake ya ufunguzi.
Naye Mwakilishi wa FAO nchini Dkt. Patrick Otto aliongeza kuwa Mwongozo huu utasaidia  kuongeza tija na kipato miongoni mwa wakulima wetu.
Dkt. Otto aliishukuru Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa kutoa ushirikiano ili kujadili mwongozo huu muhimu kwa mstakabali wa kilimo chetu.
Naye Mratibu wa warsha hii ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mazingira Bi. Shekwanandi Natai aliongeza kuwa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhakikisha kuwa inakabiliana kikamilifu na athari za tabianchi katika kilimo.
Alibainisha kuwa FAO wametoa dola 500 elfu ili kutoa msaada kwa waathirika wa mbadiliko ya tabianchi sehemu mbalimbali hapa nchini.
Warsha hii ya siku moja ilifanyika katika ukumbi wa jengo la Samaki House na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa kilimo na mazingira.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Flprence Turuka akifungua warsha

Mwakalishi wa FAO nchini Dkt.Patrick Otto akitoa hotuba
Washiriki wa warsha wakiwa katika mjadiliano ya vikundi

Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha