Wednesday, June 22, 2016

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA YAFANA KILIMO


Sherehe za Wiki ya Utumishi wa Umma zinaendelea kote nchini ambapo katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Florens Turuka aliweza kutembelea Taasisi, Idara na Vitengo vilivyopo makao makuu ya wizara hiyo, yaliyopo Temeke Jijini Dar es Salaam maarufu eneo la Vertinary ili kuonana na wafanyakazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.
Awamu ya kwanza aliweza kutembelea Idara ya Zana za Kilimo, Kitengo cha Mazingira, Mradi wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP), Mamlaka ya Kuthibiti Mbolea (TFRA) na Kitengo cha Ufuatiliaji wa Miradi ya Kilimo ( BRN).
Watumishi waliweza kumwelezea mafaniko waliyoyapata katika utendaji wao wa kazi pamoja na changamoto zinazowakabili.
Naye Dk. Turuka aliwataka kuchapa kazi kwa bidii pamoja na changamoto ndogo ndogo zinazowakabili ili kuendana na kaulimbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “ HAPA KAZI TU”.
Kwenye ziara hiyo Dk.Turuka aliaandamana na Mkurugenzi wa Utumishi na Rasilimali Watu Bw. Seushi Mburi na Mkurugenzi Msaidizi Utawala Bi. Hilda Kinanga.
Dk. Turuka ataendelea na ziara hiyo katikaTaasisi, Idara na Vitengo mbalimbali vilivyopo makao makuu ya wizara.
Katibu mkuu Frorens Turuka akisaini katika ofisi ya Idara  ya Zana za Kilimo

Dr.Turuka akiwa katika ofisi ya Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea (TFRA)