Tuesday, July 19, 2016

UNIDO Kuanzisha Viwanda vya Usindikaji wa Mazao ya Kilimo na Mifugo
Shirika la Kimataifa la uendelezaji wa viwanda (UNIDO) linajipanga kuanzisha viwanda  vya kusindika mazao yatokanayo na mbegu  kama ufuta pamba na alizeti ambavyo vitatumika katika kutengeneza malisho kwa ajili ya kunenepesha  wanyama.
Wakiongea katika kikao kilichofanyika hivi karibuni katika ofisi ya Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,na kuhusisha Idara kuu ya Kilimo,Idara kuu ya Mifugo na Wizara ya Viwanda wamesema lengo kubwa ni kuanzisha viwanda vya kusindika nyama na ngozi ambapo alizeti pamba  na ufuta vitatumika zaidi katika kunenepesha wanyama hao.
Aidha afisa uendelezaji wa viwanda UNIDO Bwana Bassel El Khatibu alisema kuwa tayari wameanzisha machinjio ya kisasa mkoani Mbeya na Iringa kwa kushirikiana na manispaa za mikoa hiyo ambapo maandalizi yanaendelea ya kutoa mafuzo kwa wafanyakazi  ili kuongeza tija katika kazi hiyo.
Aidha Mkuu wa Kitengo cha Uratibu wa Misaada ya maaendeleo mama Margaret Ndaba alisisitiza kwamba  maeneo yanayotegemewa kuendelezwa kwa mazao ya mbegu ni Dodoma,Singida,Shinyanga,Manyara na Morogoro lengo kubwa likiwa ni kuongeza thamani katika mazao hayo.
Mtaalamu wa usindikaji wa ngozi kutoka Idara kuu ya Mifugo Bwana Emmanueli John Muyiuga amewataka UNIDO kutoa mafunzo  pamoja na vitendea kazi bora katika machinjio yaliopo na yatakayo anzishwa .
"mafunzo ni muhimu sana kutolewa kwa wafanyakzi ili dhana ya uwekezaji wenye tija iweze kuwepo na wafanyakazi waweze kutumia elimu hiyo kufanya mabadiliko, katika hili tunaamini UNIDO mtalizingatia sana.Pia ni muhimu kuanzisha teknolojia za kisasa kwenye machinjio yote ili usindikaji uwe na tija. Emmanueli."
Margaret Raphael Ikongwe wa Wizara ya Viwanda na Biashara alisema ili kuweza kuongeza ushindani wa kibiashara katika mazao ya wanyama ni muhimu kuboresha malisho,machinjio pamoja na vifungashio kwani uwepo wa machinjio bora ndio upatikanaji wa nyama bora.

 Afisa maendeleo ya viwanda  wa UNIDO Bwana Bassel El Khatib akiongea na mtaalam kutoka wizara ya viwanda na Biashara (katikati) bi Margaret Raphael Ikongwe na Margaret Ndaba (kushoto) katika ofisi ya katibu wa waziri wizara ya kilimo mifugo na uvuivi wakati wa mkutano wao uliofanyika hivi karibuni.
Tuesday, July 5, 2016

TANZANIA NA JUMUIA YA NCHI ZA ULAYA WAFANYA MAZUNGUMZO YA KUBORESHA UVUVISerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jumuia ya Nchi za Ulaya ( EU) wamefanya mazungumzo ya kuwa na makubaliano ya kuboresha uvuvi.
Mazungumzo hayo yaliongozwa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles John Tizeba akisaidiana na Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi toka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohamed, upande wa Umoja wa Nchi za Jumuia ya Ulaya uliongozwa na Balozi Bw. Roeland Van De Geer
Mazungumzo yalijikita zaidi katika mkataba wa makubaliano katika uvuvi kwenye bahari kati ya Tanzania, Zanzibar na Jumuia ya Nchi za Ulaya.
Mhe. Tizeba alishauri makubaliano yatakayofikiwa yawe sawa kwa pande zote mbili ili kuweza kupata mafanikio kwa manufaa ya wadau wote.
Aidha, Mhe. Dkt. Tizeba alishauri makubaliano yatakayofikiwa yalenge katika kuelekeza nguvu kwa kuinua ufugaji wa samaki kwa wadau wa uvuvi kwa kuwa kumekuwa na upungufu mkubwa wa upatikanaji wa samaki katika eneo la maziwa kama vile Ziwa Victoria na Tanganyika.
Naye Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mohamed aliomba makubaliano yenye tija kwa kutekelezwa yatakayokubaliwa.
Balozi De Geer ameahidi kuwa EU itakuwa bega kwa bega na Tanzania katika kufanikisha makubaliano yatakayofikiwa katika mpango huo.
WAKATI HUO HUO, Mhe. Dkt. Tizeba alikutana pia na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida ambaye pamoja na kuja kijitambulisha, alifahamisha kuwa kampuni ya SUMITOMO inataka kuwekeza katika kilimo cha Pareto hapa nchini.
Bw. Yoshida alisema kampuni ya SUMITOMO kupitia kilimo cha pareto itaweza kutengeneza dawa za mbu na mbolea.
Kufuatia mazungumzo hayo kampuni ya SUMITOMO itafika wizarani Julai 14, 2016 kufanya mazungumzo na Watalaamu wa wizara ili kuona fursa za uwekezaji katika kilimo cha pareto.

Mhe.Dkt.Tizeba akiongoza mazungumzo ofisini kwake
Mhe.Dkt.Tizeba akiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Hamad Rashid Mohamed na Balozi Geer