Tuesday, August 30, 2016

UPOTEVU WA MAHINDI HUCHANGIA UHABA WA CHAKULA


Zaidi ya asilimia 30 ya zao la mahindi hupotea  baada ya na wakati wa mavuno kwa mkulima mdogo.
Hayo yalibainishwa na  mtafiti wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha  Sokoine  Profesa Valerian  Silayo wakati akiwasilisha mada katika utafiti wake alioufanya kwenye warsha ya siku moja iliyodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa  la Chakula na Kilimo (FAO),  iliyofanyika katika hoteli  ya New Afrika  Jijini Dar es Salaam.
Alifahamisha kuwa  upotevu mkubwa wa chakula hutokea wakati wa shughuli za  uvunaji, usafirishaji na uhifadhi wa mazao.
Akifafanua  hayo Silayo ameeleza kuwa uvunaji wa zao la mahindi  hutegemea sana nguvukazi watu ambao huvuna mahindi kwa kuyatupa chini hali inayosababisha upotevu  wa mahindi.
Pia katika usafirishaji wa zao hilo usafiri mkubwa unaotumika ni mkokoteni ambao huacha  kiasi kikubwa cha mahindi njiani.
"Chakula hupotea pia katika  kipindi cha uhifadhi ambapo mazao hushambuliwa na  panya, wadudu waharibifu kama dumuzi''  alisisitiza Profesa Silayo katika mada yake hiyo ya matokeo ya utafiti wake.

Utafiti huu ulifanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, ambapo vijiji kumi vilihusishwa katika utafiti huo.
Baadhi ya washiriki wakijadili mada katika warsha

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja