Sunday, September 25, 2016

ASA wafundisha Wagani 41 na Wakulima 75 Kuboresha kilimo


Zaidi ya maafisa ugani 41 na wakulima  75 wanaendelea kupata mafunzo ya kilimo bora  katika kituo cha mafunzo ya kilimo cha Mkindo ili kuweza kuboresha kilimo na kukiendesha kibiashara.
wakiongea kwa nyakati tofauti wasimamizi wa mafunzo hayo  Bwana Johnson Tillya na Jacqueline Itatiro kutoka wakala wa mbegu ASA wamesema mafunzo hayo yanalenga kuwaanda wakulima na maafisa ugani kuweza kusambaza elimu ya kilimo bora wakati wa kusimamia mashamba darasa.
Aidha mafunzo hayo ambayo yameanza tarehe 14 mpaka 27 septemba 2016 imehusisha wataalamu kutoka wilaya za Malinyi Ulanga Gairo na Morogoro Vijijini
Aidha mafunzo hayo yanalenga pia kuwapata wakulima wawezeshaji katika usimamizi wa mashamba darasa kwenye vijiji mbalimbali ndani ya halimashauri za Mkoa wa Morogoro.

Tunaamini baada ya elimu hii ya matumizi ya mbegu bora na kanuni sahihi za kilimo kusambaa kwa wakulima wa mpumga watabadilika na kufanya kilimo cha mpunga chenye tija na kupata uhakika wa masoko”. Alisema  Jacqueline