Wednesday, February 22, 2017

Third Annual Agricultural Policy ConferenceThe Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries (MALF) in partnership with the Policy Analysis Group (PAG) are jointly organizing the 3rd Annual Agricultural Policy Conference (AAPC) in Dar es Salaam, Tanzania. 
The theme for the AAPC will be “The role of agri-food systems in promoting Industrialization in Tanzania.” Scheduled to take place from 1st to 3rd March 2017, the event will bring together 150 key stakeholders in the agriculture sector from Tanzania and across the region including policy makers, researchers, farmers, NGOs, and the private sector.

Building on the success of the second Conference in 2016, the Policy Analysis Group (PAG) and the Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries (MALF) will again bring together key stakeholders working on agricultural policy projects and initiatives to discuss the challenges, opportunities, emerging issues and potential for further collaboration.

Tanzania intends to be a middle income country by 2025, to achieve this the government has placed industrialization the top of its Development Agenda. In line with this, the Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries has developed an Agro-processing Development Strategy for Tanzania which demonstrates how the agricultural sector would contribute to the national effort in achieving agriculture-led industrialization. The draft strategy will be presented during the 3rd AAPC.


Panel discussions at the 3rd AAPC will include Agriculture Sector Policy, Agricultural Trade and Marketing, Enabling Policy for Private Sector Investment, Access to Finance, Land Tenure Policy and Agriculture Input Policy. 

The third AAPC is jointly brought to you by:


Sunday, February 19, 2017

WIZARA YABADILI NJIA ZA MAWASILIANO

Kufuatia zoezi la Serikali kuhamia Makao Makuu ya nchi mkoani Dodoma Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi imebadili njia za mawasiliano kuanzia sasa baada ya kuhamia Dodoma.
Kufuatia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Utumushi na Rasilimali Watu wa Idara Kuu ya Kilimo Bw. Seushi Mburi amesema mabadiliko haya hayawezi kuepukika kwa kuwa wizara imehamia Dodoma.

Aliyataja mawasiliano hayo mapya kuwa Anuani ya Simu ni “ Kilimo Dodoma’’, Nambari za Simu ni +255 (026) 22321407 na +255 (26) 2320035, Nukushi ( Fax) ni +255 (026) 2320037 na Barua Pepe ( email) ni ps@kilimo.go.tz.

Mawasiliano mengine kwa mujibu wa Bw. Mburi ni mawasiliano ya Barua ambayo ni Idara ya Utawala, Kilimo IV Dodoma, S. L. P. 2182 Dodoma.

Ofisi mpya za Wizra zitakuwa Jengo la Kilimo IV lililopo karibu na Chuo cha VETA - Dodoma, ambapo kutakuwa na ofisi za Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Maafisa watakuwa Majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM) Block 9 Eneo la Bondeni.
Amewaomba radhi wadau na wateja wote wa wizara kufuatia mabadiliko haya kwa kuwa yanaendana na mahali ambapo wizara inafanyia kazi kwa sasa.Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi tayari wako mkoani Dodoma kuanzia tarehe 15/02/2017 wakiongozwa na Waziri wao Mhe. Dkt. Charles John Tizeba , Naibu Waziri William Ole Nasha , Katibu Mkuu Idara Kuu ya Kilimo Eng. Mathew John Mtigumwe, Katibu MKuu Idara Kuu ya Mifugo Dk. Mary Mashingo na Katibu Mkuu Idara ya Kuu ya Uvuvi Dkt. Yohana Budeba.

WAFANYAKAZI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI WAHAMIA RASMI DODOMA

Wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi leo wameaga rasmi Jijini Dar es Salaam kuhamia Dodoma ili kutekeleza agizo la Serikali la kuhamishia Makao Makuu ya Nchi mkoani Dodoma.

Wafanyakazi waliondoka katika awamu ya kwanza ni watumishi wapatao 88 kutoka Idara Kuu ya Kilimo na 120 kutoka Idara ya kuu za Mifugo na Uvuvi.

Ofisi mpya kule Dodoma zitakuwa katika jengo la Kilimo IV, Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM) na NBC.
Hafla fupi ya kuagwa imefanyika Samaki House na iliongozwa na Katibu Mkuu wa Idara Kuu ya Mifugo Dkt. Mary Mashingo, Katibu Mkuu Idara ya Uvuvi Dkt Yohana Budeba na Kaimu Katibu Mkuu wa Idara Kuu ya Kilimo Bw. Seushi Mburi.


Muda mfupi baada ya kuingia madarakani kuliongoza Taifa hili Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alitangaza rasmi nia ya dhati ya serikali yake kuhamia Dodoma ikiwa ni kutekeleza wazo la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere la mwaka 1978.


Thursday, February 2, 2017

MAGARI MENGINE YAKABIDHIWA KILIMO

Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi imepokea magaari matatu yenye thamani ya shilingi za Kitanzania zipatazo 281,220,000 kwa ajili ya Mradi wa Kuendeleza Mfumo wa Upatikanaji wa Mbegu za Mazao ya Mizizi.

Magari hayo yamepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Dkt. Hussein Mansoor kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.

Magari yametolewa na Mradi wa MEDA (Mennonite Economic Development Associates) ambapo Meneja wa Mradi wa Muhogo Bw. Stephen Magige aliweza kukabidhi. 

Bw. Magige alifahamisha kuwa magari yatatumika katika vituo 3 vinavyohusika na uatafiti wa zao la muhogo vya ARI- Kibaha, ARI- Ilonga na ARI – Ukiriguru.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Dkt. Hussein Mansoor amefahamisha kuwa mradi huo ambao umeanza Januari 1, 2017 utadumu mpaka mwaka 2021 na gharama nzima za mradi zitakuwa Dola za Marekani zipatazo 11.7 milioni.

Aidha, alifahamisha kuwa mradi unafadhiliwa na Belinda Gates kupitia MEDA ikishirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti ya IITA ( International Institute for Tropical Agriculture) pamoja na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kupitia Idara yake ya Utafiti na Maendeleo.

Mradi utaweza kuwafikia wakulima wajasiliamali wapatao 430 na pia wakulima wanufaika moja kwa moja wa mradi huo wapatao 29,000.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Dkt. Geofrey Kajiru alibainisha kuwa mbali ya wakulima wajasiliamali na wanufaika wa moja kwa moja pia ni zaidi ya wakulima milioni moja wa Tanzania wataonja manufaa ya mradi huu muhimu.

Mradi utawezesha kujenga mfumo rasmi wa uzalishaji wa mbegu za mazao ya mizizi, mfumo ambao haukuwepo hapo awali.

Pia mradi utajenga uwezo kwenye taasisi zinazohusika katika uzalishaji wa mbegu za mazao ya mizizi kama Idara ya Utafiti, TOSCI na wazalishaji binafsi.

Naye Mratibu wa Mradi wa Utafiti wa Muhogo hapa nchini Dkt. Geoffrey Mkamilo alifahamisha kuwa Mradi wa Kuendeleza Mfumo wa Upatikanaji wa Mbegu za Mazao ya Mizizi utajikita zaidi katika mikoa ya Kanda ya Mashariki ambayo itajumuisha mikoa ya Pwani, Tanga na Morogoro na Kanda ya Kusini kutakuwa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Upande wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kuna mikoa ya Mwanza, Kagera, Geita, Mara na Kigoma.

Wednesday, February 1, 2017

WAFANYAKAZI KILIMO WAPEWA MAFUNZO YA USHAURI NASAHA YA KUHAMIA DODOMA

Wafanyakazi wa Kilimo Mifugo na Uvuvi wa Idara Kuu ya Kilimo wamepata mafunzo ya ushauri nasaha juu ya kuhamia Dodoma ili kuondoa wasiwasi miongoni mwao kuhusu nia nzuri ya serikali yetu.

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kilimo 1 na yalitolewa na Watalaamu toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bi. Margaret Mussai aliwataka watumishi wanaowahamia kutokuwa na hofu hata kidogo kwani Dodoma ni sehemu ya Tanzania na mkoa unafursa kama ilivyo kwa Jiji la Dar es Salaam.

“ Naomba mje Dodoma na mtumie fursa mbalimbali zinazopatikana kwa wingi na wala hamtajuta hata kidogo” alisisitiza Bi. Mussai.

Pia alisema kuwa Tanzania si nchi ya kwanza kuhamisha makao makuu ya nchi bali kuna nchi zimefanya zoezi hili na kuleta mafanikio makubwa pasipokuwa na tatizo lolote katika nchi hizo.

Bi. Mussai alitoa mfano wa nchi jirani ya Malawi ambayo ilihamisha makao makuu ya nchi ya kutoka Blantyre kupeleka mji wa Lilongwe na pia nchi ya Nigeria ilihamisha makao makuu kwenda Abuja kutoka Lagos.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike alisema mabadiliko yoyote kwa binadamu huwa yanaleta hofu kwa mtu lakini usiyakatae mabadiliko bali lililojema ni kuyakubali madiliko.

“ Binadamu uwe tayari kukubali mabadiliko vinginevyo yanaweza kukuletea shida katika maisha yako na pengine kusababisha magonjwa kama ya shinikizo la damu” alifahamisha Bw. Golwike.

Aidha, Bw. Golwike aliongeza kuwa kukubali mabadiliko kunaweza kurefusha maisha yako hapa duniani.

Utafiti unaonyesha kuwa karibu asilimia 90 ya hofu za mtu huwa si za kweli kwani mambo huwa yanakuwa tofauti kinyume na hisia za awali za mtu kabla ya kufikia maamuzi, alifahamisha Bw. Golwike.
“Tuwe na maamuzi sahihi wakati wa kutoa maamuzi ya jambo lolote katika maisha yetu ya kila siku” alifafanua Bw. Golwike.
Bw. Golwike alimalizia kwa kuwataka watumishi wa Serikali kuwa wazalendo kwa nchi yao katika suala hili la kuhamia Dodoma.
Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Bw. Darius Damas alisema tufanye maandalizi ya kuhamia Dodoma katika familia zetu na tuachane na usiri usiokuwa na msingi kwani unaweza kuleta madhara katika jamii zetu.
Bw. Damas aliwataka watumishi kuheshimu mawazo ya muasisi wa kuhamia Dodoma Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwani alikuwa na sababu za msingi za kuamua serikali kuhamia Dodoma. 

“ Mwalimu Nyerere moja ya sababu yake kubwa ya kuhamia Dodoma ilikuwa ni kuboresha utoaji wa huduma kwa nchi nzima kwa kuwa Dodoma iko katikati ya nchi yetu” alibainisha Bw. Damas katika mchango wake.

Mchangiaji mwingine wa mada hii ni Kaimu Kamishina wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi aliwataka watumishi kuweka historia ya kuwa wa kwanza kuhamia Dodoma kwani ni jambo la fahari kwao katika kizazi kijacho.

Pia Bw. Mushi alisema ameridhika na morali iliyoonyeshwa na Watumishi wa Idara Kuu ya Kilimo kuwa kweli wanania ya dhati ya kuunga mkono maamuzi ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka serikali ihamie Dodoma kwa vitendo.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Bw. Seushi Mburi, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mafunzo haya aliwashukuru sana wawezeshaji wa mafunzo kwani yameleta hamasa kubwa na kuondoa hofu kwa watumishi kuhusu kuhamia Dodoma.

“ Mafunzo yenu yameleta mabadiliko makubwa miongoni mwetu na kupunguza sitofahamu kwa watumishi wetu na sasa wako tayari kwenda pasipokuwa na shaka “ alimalizia Bw. Mburi.