Thursday, April 27, 2017

WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI DKT. TIZEBA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI MJINI DODOMAWaziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba hivi karibu amefungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (Idara Kuu – KILIMO). Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula, Kanda ya Dodoma na kusisitiza uwajibikaji na nidhamu katika utumishi wa Umma.
 
Katika hotuba yake, Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Tizeba amesema uwajibikaji katika utumishi wa umma ndiyo chanzo cha kufanikiwa kwa Sera, Programu, Mikakati na Mipango ya Wizara. Aidha, alitoa ushauri Wizara kuwa na Baraza moja la Wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi badala ya Mabaraza mawili kama ilivyo sasa.

“Napenda niwashauri kuwepo kwa Baraza moja ambalo, litakuwa kiini cha kuwaunganisha ninyi nyote na ninaamini litakuwa na ufanisi kuliko ilivyo sasa”. Amesisitiza Waziri Tizeba.

Katika hatua nyingine, Dkt. Tizeba aliiagiza Sekretariat kuandaa mkutano ujao wa Baraza la Wafanyakazi mapema iwezekanavyo kabla ya kuanza kwa mchakato wa maandalazi ya Bajeti ya Wizara ili kutoa nafasi kwa Wajumbe na Washiriki kutoa mapendekezo na ushauri wao ili kutoa dira na miongozo kwenye vipaumbele vya Wizara kabla ya kuanza utekelezaji wa mipango mipya kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.

“Napenda pia nitoe ushauri wa kuitisha kikao cha Baraza la Wanyakazi mapema, tunapoanza kuandaa mipango ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka uliombele yetu, kwani kwa kufanya hivyo, tutatoa fursa kwa Wawakilishi wa Watumishi wa Wizara kushiriki kikamilifu na kuelewa vipaumbele vya Wizara.” Ameongeza Dkt. Tizeba.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (Idara Kuu – KILIMO) Eng. Mathew Mtigumwe ameongeza kuwa licha ya Vituo vya Utafiti, Vyuo vya Mafunzo, Idara na Vitengo kukabiliwa na changamoto mbalimbali katika utendaji wao wa kazi za kila siku ni vyema kuwe na mawasiliano ya mara kwa mara kati ya Ofisi za Wakuu wa Kanda za Utafiti, Vyuo vya Mafunzo, Idara na Vitengo mbalimbali ili kusaidia kutatua changamoto hizo mapema.

Eng. Mtigumwe aliongeza kuwa ofisi yake ipo wazi kuhakikisha kuwa anashirikiana na Viongozi wa Wizara ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa Jamii.

Mbali na mambo mengine, Wajumbe pia walipata nafasi ya kupitishwa kwenye mpango wa bajeti ya Wizara ya Fungu 43, kama ambavyo itatekelezwa kupitia Bajeti ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi ambayo inatarajia kuwasilishwa tarehe 22  Mei, 2017 Bungeni, Mjini Dodoma.


Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akipiga picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) uliofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya DodomaKatibu wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) Bwana Shanil Mayosa akimuongoza Mwenyekiti wa Balaza hilo, Katibu Mkuu, Eng. Mathew Mtigumwe kupitia ajenda za mkutano huo uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya DodomaSehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) wakisoma sehemu ya makabrasha ya mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Dodoma, hivi karibuni

Tanzania Fertilizer Regulatory Authority - Bulk Procurement: Invitation for Pre-qualification

 

TANZANIA FERTILIZER REGULATORY AUTHORITY

INVITATION FOR PRE-QUALIFICATION

PRE-QUALIFICATION NO: TFRA/PQ/2017-18/F/01

FOR BULK PROCUREMENT OF DI-AMMONIUM PHOSPHATE (DAP) AND UREA FERTILIZERS FOR THE PERIOD OF JULY, 2017 TO JUNE 2018

1.0            Tanzania Fertilizer Regulatory Authority (TFRA) has been established by the Fertilizer Act, Cap 378 and mandated by the Fertilizer (Bulk Procurement) Regulation, GN No. 49 of 2017 to coordinate importation of fertilizer through the Bulk Procurement System (BPS). The Fertilizer  (Bulk Procurement) Regulations requires the prescribed types of fertilizer to be procured under the Bulk Procurement System (BPS)

2.0            The Tanzania Fertilizer Regulatory Authority intends to Pre-qualify fertilizer dealers for procurement of fertilizer i.e DAP and UREA for Tanzania through Bulk Procurement System (BPS);

3.0            Total volume of DAP and UREA to be imported is on average of 40,000 +/-20% Metric Tons in two (2) months. Tenders shall be floated on product basis whereas the estimated quantity per two (2) months is as provided below:-

a)    DAP 15,000-20,000 MT
b)    UREA 20,000- 30,000 MT

4.0            Both locally registered companies and international companies are allowed to participate in BPS tenders.
5.0            Pre-qualification will be conducted under International Competitive Bidding (ICB), through the procedures specified in the Fertilizer (Bulk Procurement) Regulation, GN. 49 of 2017 and the Fertilizer Bulk Procurement Guidelines of 2017.
6.0            The pre-qualified bidders shall be eligible to participate in tenders for supply of DAP and UREA from   July, 2017 to  June, 2018;
7.0         A complete set of pre-qualification documents in English language can be collected by interested companies at TFRA offices by submission of a written application to the address given under paragraph 10 and upon payment of a non-refundable USD 500 by direct deposit or direct transfer or bankers cheque in favor of Tanzania Fertilizer Regulatory Authority from Monday to Friday (Working Days) between 0800 hrs and 1500 hrs.
TFRA banking details
·        Name of the bank: National Microfinance Bank PLC (NMB PLC),
·        A/c name: Tanzania Fertilizer Regulatory Authority -Fertilizers,
·        A/c number: USD Account number 20110024337,
·        SWIFT CODE: NMIBTZTZ
Bring the bank transfer documents/details or the deposit slip to TFRA office on working days (Mondays to Fridays) between 0800 hrs and 1500 hrs.

8.0            Application for pre-qualification should be submitted in sealed envelope, delivered to the address below, before or on 19th May,2017, at 1000 hrs and be clearly marked Bulk Procurement of DAP and UREA fertilizer”. Pre-qualification no. TFRA/PQ/2017-18/F/01”. Applications sent by email will not be accepted.  

9.0            Applications submitted beyond the specified time shall not be accepted
10.0       Applications will be evaluated and results be announced by 2nd June, 2017 for pre-qualified importers to participate in the tenders from   July, 2017 to  June, 2018;
11.0       Applications for pre-qualification and letter of intent should be sent to the address below.  For more clarification contact TFRA through the address provided below.   

EXECUTIVE DIRECTOR
TANZANIA FERTILIZER REGULATORY AUTHORITY (TFRA)
PADEP BUILDING,
MANDELA ROAD,
TEL+255 739 002012;
E-mail:tfra@kilimo.go.tz
DAR ES SALAAM, TANZANIA
Office hours Monday – Friday 0800 – 1500 hrs