Sunday, July 23, 2017

Katibu mkuu wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Eng Mtigumwe atembelea vituo mbali mbali vya kilimo

Katibu mkuu wizara ya Kilimo  Mifugo na Uvuvi Eng Mtigumwe akipata maelezo toka kwa wataalam wa kituo cha utafiti cholima dakawa mbegu za kisasa za mikunde na mazao mengine yanayofanyiwa utafiti kituoni hapo


 Katibu mkuu wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Eng Mtigumwe akipata maelezo ya mbegu mahindi na mtama zilizovumbuliwa kituo cha Utafiti Ilonga mkoani Morogoro


 Katibu mkuu wizara ya kilimo ,mifugo na uvuvi Eng Mtigumwe akipata maelezo ya visumbufu vya mimea kituo cha Utafiti Ilonga mkoani Morogoro


 Katibu mkuu wizara ya kilimo mifugo na uvuvi Eng Mtigumwe akiongea na watumishi wa Ari cholima dakawa mkoa wa Morogoro katika ziara yake ya kutembelea vituo mbali mbali vya wizara yake mkoani Morogoro

 katibu mkuu MALF-kilimo Eng Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kituo cha udhibiti wa panya wanaoharibu mazao kilichopo Morogoro


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo mifugo na uvuvi (idara kuu kilimo) Eng. Methew Mtigumwe (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa taasisi ya Utafita Mikocheni (ARI MIKOCHENI) Dkt. Joseph Ndunguru alipotembelea mahabara ya kilimo hivi karibuni

  
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na uvuvi (idara kuu kilimo) Eng. Methew Mtigumwe akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi ya utafiti mikocheni alipokwenda kukagua utendaji kazi wataasisi hiyo


Katibu mkuu Wizara ya Kilimo mifugo na uvuvi Eng Mtigumwe(Kushoto) akipewa maelezo jinsi ASA (Agricultural Seed Agency) wanavyotengeneza miche bora ya miembe toka kwa mkurugenzi mkuu wa ASA Dr. Mizambwa (Katikati).


 
Katibu mkuu wizara ya kilimo mifugo na uvuvi Eng Mtigumwe alipotembelea kituo cha maonyesho ya kilimo nane nane mkoani morogoro kujionea maandalizi ya maonyesho ya nane nane mwaka huu 2017 


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo mifugo na uvuvi (idara kuu kilimo) Eng. Methew Mtigumwe akiwa na wafanyakazi wa taasisi ya utafiti wa miwa kibaha (SRI), alipokwenda kukagua utendaji kazi wa taasisi hiyo

Wednesday, July 12, 2017

Mashamba Darasa Kutumika Kuwabadilisha Wakulima Mkoani Mororgoro


Wakulima Mkoani Morogoro wametakiwa kutembelea mashamba darasa na kuwafuata maafisa ugani ili kujifunza namana bora ya uzalishaji wa mazao hasa mpunga.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja Uzalishaji Bwana Charles Levi wakati wa sherrehe za siku ya mkulima iliyofanyika  Wilaya ya Mvomero katika kijiji cha Mkindo amesema wakulima ambao hawajapata mafunzo wanatakiwa kutembelea mashamba darasa na kuomba ushauri kwa wataalamu wa kilimo walio karibu nao ili kuboresha mbinu zao za uzalishaji katika kilimo
Aidha Bwana Levi amesema kuwa wameanzisha mashamba darasa katika Wilaya zote Mkoani Morogoro kwa lengo la kuwahamasisha wakulima kutumia mbegu bora za kilimo na mbinu za kisasa za uzalishaji
 Bwana Levi ameeleza kwamba katika mashamba darasa hayo  Wakala wa Uzalishaji wa Mbegu (ASA) walitoa aina mbalimbali za mbegu zikiwemo TXD 306, Nerica 1,Nerika 4,Nerika 7,komboka, supa na Mwangaza ambapo wakulima hutakiwa kuchagua aina moja au mbili za mbegu ambazo wamezipenda.
Hata hivyo Wilaya ya Mvomero wakulima wengi wamechagua  mbegu aina ya Komboka Saro pamoja na Supa kutokana na uzaaji,upachaji na ustahimilivu wa  ukame zilizo nazo’ alisema Bwana Levi
Aidha Wakala imejipanga kuwatumia mabwanashamba, vyombo vya habari na wakulima viongozi katika kuwahamasisha wakulima kutumia mbegu bora pamoja na mbinu za kisasa za uzalishaji.
Katika kuimarisha Zoezi la usambazaji wa mbegu wakala Kupitia taasisi na wataalam mbalimbali tumefanya  tafiti ili kubaini mahitaji halisi na kalenda za kilimo kwa kila eneo ili kuweza kusambaza mbegu hizo kwa wakati, alisisitiza Bwana Levi
Halima Hamisi ni Mkulima wa Kikundi cha Ushauri anasema ASA wamewasadia kupata mbegu bora kama Komboka na Mwangaza ambazo hizo ndizo tunazitegemea sana kutuondoa katika umaskini kwa kuwa  zinzaa sana zinahimili ukame na zinakomaa mapema
Kutokana na elimu niliyopata  nategemea msimu wa kilimo unaokuja nitalima shamba langu mwenyewe na nitayatumia mafunzo haya kuhakikisha najikwamua na umaskini, alisema Halima