Thursday, August 17, 2017

Maandalizi ya Siku ya Chakula Duniani - Geita


Kikao cha siku ya chakula duniani inayofanyika oktoba 10 mpaka 16 kila mwaka kimeendelea tena  katika ukumbi wa Kilimo I Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi leo.
Katika kikao kazi hicho Mwenyekiti wa kamati ya maonesho Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usalama wa Chakula Mama Amolo Juma amesema maadhimisho hayo yatatumika kuonesha teknolojia za kisasa ambazo zitawasaidia wakulima wafugaji na wavuvi katika upatikanaji wa usalama wa chakula .
Aidha maonesho hayo yatafanyika katika mkoa wa Geita na Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni badili mwelekeo wa uhamaji: wekeza katika Usalama wa Chakula na Maendeleo Vijijini
Wadau wote wanaohusika  na shughuli zote za Kilimo Mifugo na Uvuvi wanatakiwa kuanza maandalizi ya namna ya kushiriki katika maadhimisho hayo  alisema mwenyeketi mama Amolo.

Tuesday, August 8, 2017

Wakulima wametakiwa kuzalisha malighafi za viwandaniWakulima wametakiwa kuzalisha kwa tija malighafi za viwandani kwa wingi katika kilimo ili kuchangia katika uanzishwaji wa viwanda hapa nchini
Akiongea katika siku ya kilele cha maadhimisho ya Nanenane yaliofanyika ki taifa Mkoani Lindi katika viwanja vya vya Ngongo Waziri wa Kilimo Mifugo na uvuvi Mhe. Chales Tzeba amewataka wakulima  kulima kwa wingi malighafi ambazo zitatumika katika viwanda ambavyo vinaanzishwa sasa
Awali akizungumzia  kuhusu changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa waziri amesema kuwa watafiti tayari wamegundua teknolojia mbalimbali ambazo zinapambana na mabadiliko ya tabianchi hivyo kuwataka wakulima kutumia teknolojia hizo ili kuongeza tija katika kilimo.
Aidha kutokana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi wizara ya kilimo mifugo nja uvuvi tayari imeandaa miongozo mbambali kutegemeana na hali ya kanda husika alisema Mhe. Tzeba.

Tumieni Utajiri wa korosho kubadilisha maisha yanu

Wakulima mkoani Lindi na Mtwara wametakiwa kutumia pesa za korosho walizopata katika msimu wa 2016/2017 kuboresha maisha yao.
Akihutubia mamia ya wakulima wafugaji na wavuvi waliohudhuria kufungwa kwa maadhimisho ya Nanenane 2017 Makum wa Rais Mama Samia Suluhu amewataka wananchi wa Lindi na Mtwara kutumia pesa walizopata kujenga makazi bora,kusomesha watoto na kununua chakula cha kutosha familia zao
Aidha amewasifia wakulima hao kwa namna ambavyo wameweza kupokea   teknolojia za kilimo hivyo kubadilisha sura ya maonesho ikilinganishwa na maonesho ya mwaka jana

Monday, August 7, 2017

Watafiti wa korosho watakiwa kuunganisha uzalishaji na soko

Watafiti wa zao la korosho wametakiwa kuunganisha utafiti na masoko ili kuwasaidia wakulima wakati wa uongezaji wa thamani ya mazao yao
Akiongea wakati alipotembelea  mabanda ya Kituo cha  utafiti cha  Naliendele Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt Chales Tzeba amesema namna pekee ya kuwasaidia wakulima wa korosho ni kuwapa elimu juu ya  teknolojia za usindikaji na uongezaji wa thamanai wa bidhaa zitokanazo na korosho na kuwaunganisha na masoko.
mmekuwa mkifanya tafiti nyingi na kubwa kwa zao la korosho na mhogo sasa utafiti wenu usiishie kwenye kutafiti wa teknolojia za uzalishaji pekee lakini muweze kuwaunganisha wakulima soko na uongezaji wa thamani wa bidhaa zitokanazo na tafiti zenu.” alilisistiza Mhe. Tzeba.
Aidha amesema serikali imekuwa ikijitahidi kutoa ruzuku za pembejeo na kufuta kodi ambazo zilikuwa ni kikwazo kwa wakulima lengo likiwa ni kumnyanyua mkulima mdogo

Wakulima watakiwa kuongeza uzalishaji wa zao la nganoWakulima watakiwa kuongeza uzalishaji wa ngano ili kukidhi mahitaji ya soko na kuachana na uangizaji wa zao hilo nje ya nchi
Akiongea leo wakati wa maonesho ya Nanenane 2017  yaliofanyika kitaifa Mkoani Lindi katika Uwanja wa Ngogo Mhe,Hamadi Rashidi Mohamedi Waziri wa Kilimo Maliaasili,Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema uagizwaji wa ngano kutoka nje unatumia fedha nyingi za kigeni ambazo zikilinganishwa na thamani ya pesa ya kitanzania ni hasara kubwa kwa serikali.
“Serikali inatilia mkazo uuzwaji wa bidhaa za kilimo nje ya nchi la ili kupata fedha za kigeni kuliko uagizaji wa bidhaa kutoka nnje ambazo kimsingi thamani yake ni ndogo katika nchi “ . Alisema  Mhe. Waziri
Aidha ngano ni zao pekee linaloagizwa kutoka nchi za nje kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na mazao mengine kutokana na wakulima wengi kutotilia mkazo na umuhimu wa zao hili.
uzalishaji wa ngano hapa nchini ni tani 50,467 na mahitaji kwa mwaka ni tani 251,396 hivyo  kuna kila sababu kwa wakulima kuongeza uzalisha wa zao hilo ili kukamilisha mahitaji ya soko
Naye Mkurugenzi msaidizi Idara ya Usalama wa Chakula Bi Josephine Amolo amesema nchi imejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 123 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo baadhi ya halimashauri zilionekana kuwa na uhaba wa chakula.
Wakulima watakiwa kuongeza uzalishaji wa zao la nganoWaziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Charles Tzeba akisalimiana na  Waziri wa Kilimo Maliaasili,Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanziba Mhe.Mhe,Hamadi Rashidi Mohamedi alipotembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo naUuvuvi (kilimo) leo


 


Mhe,Hamadi Rashidi Mohamedi Waziri wa Kilimo Maliaasili,Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usalama wa Chakula Bi Josephine Amolo wakati alipotembelea mabanda ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi  leo