Friday, November 24, 2017

ASDPII Kuleta mabadiliko makubwa ya Sekta ya Kilimo




Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo  awamu ya pili (ASDPII) imejipanga kuimarisha matumizi ya maji, kuongeza uzalishaji na tija, uongezaji wa thamani za mazao na kutengeneza mazingira wezeshi
Akiongea kwenye  Kituo cha Taifa cha Matangazo cha TBC -1 wakati wa kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa kila siku ya Alhamisi Waziri wa Kilimo Mheshimiwa  Dkt.Charles Tizeba  amesema Tanzania kuna mvua za kutosha lakini hapakuwa na utaratibu wa kuyahidhi maji yasipotee lakini ASDPII imekuja na kipaumbele cha matumizi bora ya  maji, kuongeza uzalishaji na tija, uongezaji wa thamani za mazao na kutengeneza mazingira wezeshi.
Aidha ifikapo 2021 kupitia program ya uendelezaji wa kilimo endapo ikitekel;ezwa vizuri kilimo kitachangia kwenye ukuaji wa uchumi kwa zaidi ya 40% ikilinganishwa na 29 ya sasa alisema Mheshimiwa  Charles Tizeba.
Tofauti na mwanzo kwa sasa ASDP II imewahusisha Wizara ya Kilimo,Maji na umwagiliaji, Mifugo na Uvuvi TAMISEMI na wadau wa wote wa kilimo ili kuhakikisha kuwa kilimo kinazalisha malighafi za kutosha katika kipindi hiki cha uchumi wa viwanda alisistiza Dkt. Tizeba.

Benki zatakiwa kuwakopesha wanunuzi na wasindikaji wa mazao ya kilimo





Waziri wa Kilimo Mheshimiwa  Charles Tizeba  amezitaka Benki zikiwemo Benki ya Kilimo,CRDB,na NMB kuwakopesha wanunuzi wa mazao ya kilimo, wasindikaji, na wakulima wenyewe kwa kuwa wanategemeana
Akiongea kwenye  Kituo cha Taifa cha Matangazo cha TBC -1 wakati wa kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa kila siku ya Alhamisi amesema mkulima ana wadau muhimu wanaomzunguka ambao wakipata mikopo wanaweza kukifanya kilimo kiwe na  tija zaidi.
Wanunuzi wa mazao ya kilimo na wasindikiaji wa mazao hayo wana nafasi kubwa katika kuongeza soko la mkulima wa Tanzania alisema Mheshimiwa Charles Tizeba  .
Aidha amepongeza Taasisi hizo za CRDB na NMB kwa namna walivyoweza kuwakopesha wakulima  katika misimu ya kilimo iliyopita na kuwataka wakulima kujiunga katika vikundi ili waweze kukopeshaka.
Amewataka wakulima kusindika mazao yao kabla ya kuyauza ili waweze kufaidika na kuwa chanzo cha wazalishaji wa mali ghafi za viwandani hapa nchini.

Friday, November 17, 2017

NKM akutana na watumishi Kilimo.







Watumishi wa Wizara ya Kilimo wametakiwa kufanya kazi kwa ushirkiano mkubwa  ili kuweza kuyafikia malengo  waliojiwekea na kuinua sekta ya kilimo hapa nchini
Akiongea baada ya utambulisho uliongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bi Janeth Simkanga, Naibu Katibu Mkuu Dkt.  Thomas Kashililah amesema ushirikiano baina ya wafanyakazi na viongozi  ndio chanzo cha mafanikio ya sekta ya kilimo
Aidha amewapongeza watumishi hao na kuwatakia safari njema kwa  wale wote wanahamia Dododma.

Thursday, November 16, 2017

Kilimo Kuwashirikisha Farm Africa kwenye ASDP II




Mkurugenzi wa  Sera na Mipango Bi Janeth Simkanga akiongea jambo wakati wa mkutano wa mashirikiano baina ya Wizara ya Kilimo na Farm Africa uliofanyika katika ukumbi wa kilimo I hivi karibuni



Wizara ya Kilimo imekutana na Shirika linaloshughulikia kilimo la Farm Africa lengo likiwa ni kuona namna bora ya kushirikiana katika kuendeleza sekta ya kilimo hapa nchini.

Akiongea kwenye mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Kilimo I hivi karibuni, Mkurugenzi wa  Sera na Mipango Bi Janeth Simkanga amesema Shirika hilo limekuwa likifanya shughuli nyingi za kilimo  ikiwemo kupeleka teknolojia, kutafuta masoko ya wakulima na kuongeza thamani ya mazao katika mikoa mbalimbali ikiwemo Manyara, Tabora na Arusha lakini hapakuwa na ushirikiano na Wizara ya Kilimo.
Alisema  imefika wakati wa Wizara ya Kilimo kuwatambua wadau wake na kujua wanachokizalisha  ili waweze kuingia katika mfumo wa program yakitaifa ya  kuendeleza kilimo hapa nchini (ASDP II)
Mkurugenzi wa kampuni hiyo hapa nchini Bwana Stive Ball wakati wa wasilisho lake amesema shirika hilo linashughulika na uendelezaji wa kilimo na maliasili, uongezaji wa thamani ya mazao, matumizi ya Tehema (ICT) katika kuendeleza kilimo, uhifadhi wa mazingira  (CSA) na utafutaji wa masoko ya wakulima.
Aidha shirika hili limekuwa lishughulikia mazao ya mahindi, mpunga, ufuta, maharage na Uyoga  na wamekuwa wakishirikiana na vituo mbalimbali vya Utafiti wa Kilimo pamoja na Wakala wa Mbegu wa Taifa (ASA) ili kupata mbegu bora alisema bwana Stive.

Naye Tumaini Elibariki Meneja wa Programu wa Shirika hilo amesema wakulima wengi wamepata mafunzo juu ya matumizi ya simu za kisasa (smart phone) ambazo zimewekewa programu maalum yenye kufundisha namna mbalimbali kuhudumia mazao.
Aidha kufuatia teknolojia hiyo  wakulima wameweza kufundishana kupitia simu hizo na  tija kubwa imepatikana alisisitiza Bwana Tumaini.
 Tumaini Elibariki Meneja wa Programu wa Shirik Farm Africa akionesha namna wanavyotoa  mafunzo juu ya matumizi ya simu za kisasa (smart phone) ambazo zimewekewa programu maalum yenye kufundisha namna mbalimbali kuhudumia mazao.


Sunday, November 12, 2017

MHANDISI MTIGUMWE ATANGAZA KIAMA KWA MAAFISA UGANI NCHINI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Taasisi ya HORTI Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika Ofisi za Taasisi ya Horti Tengeru na Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI Tengeru). Mwingine ni
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utafiti Dkt Mansoor Hussein
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Taasisi ya Horti Tengeru na Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI Tengeru).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI-Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi
Afisa Mfawidhi -HORTI-Tengeru akisoma Risala kwa niaba ya watumishi wenzanke wakati wa kikao cha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya HORTI  Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.
Afisa Mkuu wa Utafiti wa Kilimo Bi Alice M. Kavishe akichangia mada wakati wa kikao cha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.
Afisa Mkuu wa Utafiti wa Kilimo Dkt Stephen Sebastian Kuoko akichangia mada wakati wa kikao cha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI  Tengeru).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.

Na Mathias Canal, Arusha
Serikali imekuwa ikiongeza idadi ya wanafunzi katika Vyuo vya Kilimo na kwa sababu hiyo Maafisa Ugani wamekuwa wakiongezeka kila mwaka ambapo hali hiyo imewezesha Karibu kila Kata hapa nchini kuwa na Afisa Ugani.
Lakini pamoja na kuwepo kwa wataalamu hao wa kilimo bado uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini yakiwemo mazao ya chakula na biashara si wa kuridhisha ambapo wakulima wanalima na kupanda pasina hata kufuata hatua za kitaalamu.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi akizungumza na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI TENGERU) kilichopo katika Kijiji cha Tengeru, Kata Patandi, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.
Alisema lengo la Serikali kusambaza  Maafisa Ugani kwenye Halmashauri mbali mbali nchini ilikuwa  kuwasaidia  wakulima  waweze kufanya Kilimo kwa Ufanisi na kuongeza mavuno.
Hata hivyo jambo hilo limekuwa kinyume kwani asilimia kubwa ya maafisa ugani ama hawafanyi kazi zao ipasavyo ama wameshindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo.
Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Wizara ya kilimo inaandaa utaratibu wa kuwarudisha shule maafisa ugani wasiofaa kutokana na uchache wa ellimu zao na uwajibikaji huku wale ambao watashindwa kabisa kuwa msaada kwa wakulima baada ya masomo wizara itapendekeza waondolewe kazini.
Alisema Maafisa ugani hao Watafanyiwa usaili upya ili kubaini uwezo wao kwani wengi wao wameajiriwa na serikali lakini wakulima hawanufaiki na kilimo tafsiri yake Wataalamu hao ama hawatekelezi wajibu wao au hawana uwezo wa kutekeleza ipasavyo.
Aidha, alisema Maafisa ugani kote nchini wanatakiwa kuwekeza kwenye utoaji wa Huduma ya  Ugani kwa Wakulima  ili iwe rahisi kwa Mkulima kusaidika katika uzalishaji wa mazao mbalimbali ya biashara na kilimo.
Sambamba na hayo pia aliwasihi Wakufunzi katika chuo hicho kujiendeleza kielimu huku akisema kuwa Wizara ya kilimo lazima itengeneze mpango wa kuwaendeleza wakufunzi ili kuzalisha wataalamu wenye ufanisi zaidi.
Alisema anatambua kuwa Mahitaji ni makubwa katika vyuo vya kilimo hivyo Wizara inatazama namna ya kuongeza chuo kingine kama hicho huku akiwasisitiza wataalamu hao kubadili mfumo badala ya kusoma kwa jumla masomo mengi na kufikia hatua ya kuchagua eneo maalumu la kusoma (Kozi) kwani Kilimo ni somo pana.
“Nategemea muandae mpango maalumu ambao utapelekea Kuwa na kozi za muda mchache sio lazima kuwa na kozi za muda mrefu pekee kama ilivyo hivi sasa” Alisema Mhandisi Mtigumwe
Katika hatua nyingine amewataka Watumishi wote kuongeza spidi katika utendaji wa kazi ili kuunga mkono juhudi za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali ya awamu ya tano yenye kauli mbiu ya HapaKaziTu.
Sambamba na kutembelea na kuzungumza na watumishi na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mbogamatunda na Maua (HORTI TENGERU) Akiwa ziarani Mkoani Arusha Katibu Mkuu Mhandisi Methew Mtigumwe alitembelea pia Taasisi ya Utafiti Horti Tengeru, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kaskazini (NZARDI) na Taasisi ya Utafiti ya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki.
MWISHO