Monday, August 13, 2018

UWEKEZAJI HAFIFU KATIKA TAFITI ZA KILIMO CHANZO CHA TIJA NDOGO KWA WAKULIMA


 Kaimu mkurungenzi mtendaji waTaasisi ya kilimo TARI Dkt. Degratius Rwezaura  akiongea na watafiti walihudhuria mkuatano wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa NFRA Dodoma

Uwepo wa tija ndogo katika Sekta ya kilimo na taknolojia chache hapa nchini kumetokana na kutengewa kiasi kidogo cha fedha kutoka serikalini na kwa wadau wa maendeleo. Hayo yamesemwa na kaimu mtendaji mkuu wa taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI Dkt Degratius Rwezaura ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano uliowakutanisha watafiti wa kilimo na mifugo uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa wakala wa uhifadhi wa chakula wa taifa NFRA uliopo Dodoma.
Dkt Rwezaura amesema kwamba fedha zinzotengwa na serikali kwa ajili kufanya utafiti wa kilimo zimekuwa ndogo hivyo kushindwa kukamilisha lengo la watafiti kubuni teknolojia mbaliambali za kilimo na mifugo ambazo ni muhimu sana katika kipindi hiki cha uchumi viwanda

Aidha Dkt Rwezaura amesema utafiti wa kilimo na mifugo hapa nchini umekuwa ukigharimu kiasi kikubwa cha fedha kwakuwa uwekezaji katika miundombinu ya utafiti ikiwemo ujenzi wa vyumba vya baridi vya kuhifadhi mbegu(cold room) na mahabara za kutosha haujafanyika kikamilifu hivyo kulazimu kuendelea kuhifadhi mbegu katika vitalu kwa kulilima kila mwaka

. “Kama tungekuwa na mahabara jini tungeweza kuifadhi na kusambaza mbegu bora za kilimo na mifugo kwa wakati badala ya kulima kwenye vitalu kila mwaka ili kuepuka kuharibika kwa mbegu.” Allisema Dkt. Rwezaura

Hata hivyo amebainisha kwamba takwimu zinaonesha kuwa Serikali imenachangia asilimia 0.17 katika uwekezaji kwenye utafiti ikilinganishwa na nchi nyingine kama Uganda na Kenya ambazo katika utafiti wamewekezeza asilimia 4.6 alisema Dkt. Rwezaura

 “Kilimo chetu kimeendelea kukosa tija kwa sababu ya uwekezaji mdogo wa fedha kutoka kwa wafadhili na serikali ”alisistiza Dkt Rwezaura

Aidha Dkt. Rwezaura alimalizia kwa kusema kwamba lengo la mkutano huo ni kutengeneza hoja na kukutana na watunga sera ili kuweza kutafuta fedha za kuendeleza utafiti wa kilimo na mifugo kwa ajili ya upatikanaji wa malighafi za viwandani

 Naye Dkt Bakari Msangi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) amesema kwamba Taasisi hiyo imeratibu tafiti nyingi hapa nchini kupitia mfuko wa serikali hasa katika sekta ya kilimo mifugo na uvuvi lengo likiwa ni kurahisisha ufanywaji wa tafiti mbalimbali.

Aidha Dkt Msangi amebainisha kwamba watafifi wapatao 517 walijengewa uwezo kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia katika kiwango cha uzamili na uzamivu lengo ni kuwafanya waweze kuimarisha sekta ya kilimo

Hata hivyo Dkt Msangi amesisitiza kwamba kuanzia mwaka 2010-16 wameweza kupeleka kiasi cha shilingi bilioni 5. 1 kwa watafiti kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya utafiti ikiwemo ujenzi wa mahabara katika maeneo ya Zanzibari,makutopora Dodoma, Mpwapwa Naliendele na katika Mikoa ya wa Kilimanjaro.

Amesema COSTECH wamekuwa wakiratibu ujenzi wa miundombinu ya utafiti kwa sababu ya umuhimu mkubwa wa mazingira bora katika ufanyaji wa utafiti Aidha ametoa wito kwa watafiti kufanya tafiti zenye ubunifu ili kuendana na mahitaji na kuwafikiwa walengwa kwa wakati.

 utafi kwa sasa unatakiwa kwenda na ubunifu kwa sababu mazao ya utati yapo mengi lakini haziendi mara kwa watumiaji kutokana na kutotumika kwa ubunifu wa kutosha hivyo kwa sasa tunasisitiza sana ubunifu kwenye tafiti ili ziweze kuwavutia walengwa. Alisema Dkt Msangi. mwisho