Thursday, October 25, 2018

DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO


Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mtambo wa kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018. Mwingine Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh Pandit. 
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakifatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), alipotembelea na kukagua kiwanda cha Darsh jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.


Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), amewataka wakulima wa nyanya Mkoani Iringa kuchangamkia fursa ya kuongeza uzalishaji wa nyanya ili kuakisi uhitaji wa viwanda vya nyanya ikiwa ni pamoja na kiwanda cha Darsh chenye uwezo wa kusindika Tani 250 za nyanya kwa siku.

Waziri Tizeba ametoa mwito huo jana Octoba 18, 2018 wakati akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Kiwanda hicho kinafanya shughuli za ukusanyaji wa nyanya kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa na mikoa ya jirani na kufanya usindikaji wa nyanya ambapo hupeleka kiwanda cha Arusha kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na nyanya ambazo huuzwa ndani na nje ya nchi.

Waziri Tizeba, aliwataka wakulima hao kujiunga kuanzisha kikundi cha ushirika ili kuwa na urahisi wa mikopo ili kuwezesha uwezo wa uwekezaji kupitia kilimo cha umwagiliaji kitakachoongeza tija katika kipato chao na jamii kwa ujumla.

“Wakulima wa nyanya hapa Igwachanya na hata katika maeneo mengi nchini wanalima kwa kutegemea mvua na uzalishaji huwa mdogo na usiokidhi mahitaji ya soko hivyo nawasihi kuongeza uzalishaji wa nyanya kwani soko la uhakika lipo” Alikaririwa Dkt Tizeba

Kadhalika, Waziri wa kilimo aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuongeza wigo wa ununuzi wa nyanya katika mikoa mingine ya uzalishaji ikiwemo mkoa wa Dodoama na Singida.

Awali akisoma taarifa ya kiwanda hicho mbele ya mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh Pandit ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhimiza sera ya uchumi wa viwanda kwa kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto chache zinazojitokeza hivyo kuendelea kulinda maslahi mapana ya Taifa.

Alisema uanzishwaji wa kiwanda hicho ulitokana na ushawishi uliopatikana kutoka kwenye muunganiko wa wajasiliamali vijijini (MUVI) na Techno Serve walipotembelea kiwanda cha Darsh Mkoani Arusha.

Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela alimpongeza waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba kwa kutenga muda wake na kukubali kufanya ziara Wilayani Iringa ili kubaini changamoto zinazowakabili wakulima wa nyanya nchini.

MWISHO.

“SERIKALI KUCHUKUA HATUA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZINAZOVIKABILI VYAMA VYA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO” -DKT TIZEBA

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza umuhimu wa SACCOS nchini wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Sehemu ya wanachama wa vikundi vya akiba na mikopo wakifatilia hotuba ya Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Willium Vangimembe Lukuvi (Mb) mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania imeendelea kuchukua hatua stahiki katika kukabiliana na changamoto zinazovikabili vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vinaleta tija kwa jamii.

Hatua zilizochukuliwa na serikali ni pamoja na kuchukua hatua za kiutawala na kidola kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo waliojihusisha na wizi na ubadhirifu wa fedha katika vyama hivi, mfano; Alayabe SACCOS cha  Karatu Mkoani Arusha, Mbinga Teachers SACCOS Mkoani Ruvuma na Ulanga Teachers SACCOS Mkoani Morogoro ambako baadhi ya viongozi na watendaji wamefikishwa mahakamani kwa vitendo vya ubadhirifu.

Vilevile, Kutengeneza mikakati ya kuhakikisha kwamba vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo haviendelei kutengeneza madeni yasiyokuwa na tija kwa jamii na kusaidia kuweka mikakati ya kupunguza madeni ambayo tayari yapo katika vyama vyetu vya ushirika wa Akiba na Mikopo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.

Waziri Tizeba alisema kuwa serikali imeanza kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na waajiri kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali kwa ajili ya kuwahimiza waone umuhimu wa kuwasilisha kwa wakati makato wanayokata kutoka katika mishahara ya watumishi waliokopa katika SACCOS ili fedha hizo ziweze kutumika kwa shughuli za maendeleo zilizokusudiwa.

Alisema pia, serikali itaendelea kuendesha mafunzo mbalimbali kwa viongozi, watendaji na wanachama wa vyama vya ushirika vya Akiba na Mikopo ili waweze kufahamu miongozo na taratibu mbalimbali za utendaji wa vyama hivi ili hatimaye viweze kuleta tija iliyokusudiwa kwa jamii inayozunguka.

Katika utafiti uliofanyika katika siku za hivi karibuni umebaini kwamba Tanzania ina jumla ya vyama vya ushirika vya Akiba na Mikopo 5640 kati ya vyama 55000 sawa na asilimia 10.3 ya vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo Duniani.

Kwa mujibu wa utafiti huo, Tanzania ina jumla ya wanachama wapatao milioni moja na laki nane kwa SACCOS zote nchini kati ya wanachama milioni miambili (200) ya wanachama wote wa SACCOS sawa na asilimia 0.9 ya wanachama wa SACCOS zote Duniani.

Dkt Tizeba alisisitiza kuwa Licha ya uchache wa wanachama wake ukilinganisha na idadi ya wanachama Duniani, SACCOS hapa nchini Tanzania zimeendelea kuwa msaada na mkombozi mkubwa katika kuondoa umasikini wa wanachama wa vyama hivi na jamii kwa ujumla wake.

Aidha, alisema Sekta ya ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) imeendelea kupanuka katika nchini kufuatia kuanzishwa kwa SACCOS nyingi katika maeneo ya mijini na vijijini hali ambayo imechangia kuongeza huduma ya kifedha kwa wananchi wa kawaida na hivyo kuleta tija kwa jamii.

Sambamba na hayo, alieleza kuwa uwepo wa maendeleo ya ushirika wa Akiba na Mikopo nchini umesaidia wanachama wengi kujijengea utamaduni wa kuweka akiba ya fedha mara kwa mara na kuwa na matumizi bora ya fedha wanazoweka akiba. Vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) vimechangia kujenga tabia ya kujiamini na kuaminiana kifedha miongoni mwa wananchi wa kawaida na kujenga.

MWISHO.

DKT TIZEBA ALITAKA JESHI LA POLISI KUTOA TAARIFA SAHIHI ZA AJALI YA WATUMISHI WATANO ILIYOTOKEA MKOANI SINGIDA

div class="separator" style="clear: both; text-align: center;">
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akiongoza zoezi la kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida, Wengine pichani ni Waziri wa fedha na Mipango Mhe Philiph Mpango, Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa, na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega. 
Sehemu ya waombolezaji walioshiriki kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza wakati wa kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akiwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakati wa kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa taarifa za miili ya marehemu wakati wa zoaezi la kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na rasilimali watu Bi Hilda Kinanga akieleza hatua zilizochukuliwa na wizara ya kilimo tangu kutokea ajali iliyoua watumishi watano wa wizara hiyo katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) leo Jumanne tarehe 23 Octoba 2018 ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida wakiwa safarini kutokea Jijini Dodoma kuelekea mkoani Shinyanga na Mwanza kikazi.

Ajali hiyo iliyolihusisha Lori la mizigo na gari ya serikali STK 8925 iliyokuwa na watumishi hao watano ambao walikuwa safarini kuungana na Ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya afrika (AFDB) kwa maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kuanzisha viwanda vya kusindika mazao (Stage Agro Processing Zone).

Dkt Tizeba amelitaka jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kutoa taarifa zilizo sahihi tofauti na taarifa walizozitoa awali za ajali hiyo kwani zinakinzana na maelezo ya dereva wa Lori ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni vilevile kukinzana na maelezo yanayotolewa na mashuhuda waliopo katika eneo la ajali hiyo.

“Naomba Kauli iliyotolewa na jeshi la polisi irudiwe tena waende wakafanye utafiti wa kweli kwani kumekuwa na lawama kwa dereva wa serikali ambazo hazistahili maana taarifa zinasema kuwa dereva wa Lori alikuwa anaingia barabarani pasina kufuata taratibu jambo lililopelekea kutokea kwa ajali hiyo”

“Ninaomba sana jeshi la polisi kutenda haki katika tukio hili lenye kuacha maumivu kwa familia, wizara na Taifa zima” Alikaririwa Dkt Tizeba

Waziri Tizeba amewataka wananchi kuacha kulaumu na kutoa hukumu kwa dereva wa serikali kwa kusababisha ajali hiyo badala yake kuwaombea marehemu wapumzike kwa amani kwani hakuna binadamu anayeweza kusababisha ajali na vifo vya watu wengi kwa makusudi.

Watumishi hao walioagwa kwa kupoteza maisha kwa ajali ya gari ni Dereva Mwandamizi wa wizara ya kilimo Ndg Abdallah Seleman Mushumbusi (53), Afisa kilimo wa Wizara Ndg Charles Joseph Somi (33), Mkemia daraja kwanza Ndg Erasto Isack Mhina (43), Mtakwimu daraja la kwanza Bi Ester Tadayo Mutatembwa (36) na Mhasibu daraja la pili Bi Stella Joram Ossano (39).

Aidha, Mhandisi Tizeba ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watumishi wote wa wizara ya kilimo kwa kupoteza nguvu kazi ya Taifa tena watumishi hao wakiwa safarini kutekeleza majukumu ya kiserikali.

Vilevile amewashukuru wabunge wa kamati ya kudumu ya maji, kilimo na mifugo kwa kuacha kikao kazi ili kuungana na waombolezaji kuaga miili ya watumishi hao.

Viongozi wengine walioshiriki katika zoezi la kuaga miili hiyo ni pamoja na waziri wa fedha na Mipango Mhe Philiph Mpango, Waziri wa Viwanda, Bishara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage, Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe amewataja watumishi hao waliofariki kuwa walikuwa wachapakazi hodari, wapole, wacheshi na waadilifu hivyo kufuatia mauti iliyowakumba Wizara imepata pengo kubwa.

Alisema kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma mwajiri anagharamia misiba hiyo na kuahidi kushirikiana na ndugu wa marehemu kwa ajili ya taratibu nyingine za kupata haki na mafao yao.

MWISHO

SIMIYU: DKT TIZEBA ATEMBELEA MAONESHO YA SIDO ASISITIZA UMUHIMU WA VIWANDA VIDOGO NCHINI

div class="separator" style="clear: both; text-align: center;">
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba  (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa Mara baada ya kuwasili Mkoani Simiyu kwa ziara ya kikazi ya siku moja, leo Alhamisi Octoba 2018. 
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba  (Mb) akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza jambo mara baada ya kuwasili kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza jambo wakati akikagua mashine zinazotengenezwa na SIDO TDC kwa ajili ya uchakataji wa mazao mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.SIMIYU: DKT TIZEBA ATEMBELEA MAONESHO YA SIDO ASISITIZA UMUHIMU WA VIWANDA VIDOGO NCHINI

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba  (Mb) leo Alhamisi Octoba 2018 amewataka wajasiriamali kote nchini kuchangamkia fursa ya kutembelea katika Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Katika maonesho hayo ambayo yalianza Oktoba 23 mwaka huu, Dkt Tizeba amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wananchi kuweza kujielimisha katika maeneo mbalimbali ya teknolojia za viwanda hususani viwanda vidogo, lakini pia wajasiriamali kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa maeneo mengine nchini na nje ya nchi.

"Nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani kama Mara, Mwanza na Shinyanga wajitokeza  kwa wingi kushiriki maonesho haya maana hii ni fursa muhimu kwao katika kuakisi kwa vitendo Tanzania ya viwanda" Alisema Dkt Tizeba

Dkt Tizeba amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kwa kubuni jambo hilo sambamba na kumpongeza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage kwa kuwaalika wajasiriamali, na wataalamu waoneshaji wa teknolojia mbalimbali kwani jambo hilo litatoa fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine kuona ushindani katika uongezaji wa thamani wa mazao mbalimbali na fursa kwa wajasiriamali kujifunza kutoka kwa wenzao.

Aidha, Dkt Tizeba amesema kuwa Maonesho hayo ya SIDO ambayo ni ya kwanza kufanyika Kitaifa yatawasaidia wajasiriamali kote nchini kupanua masoko ya bidhaa zao.

Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO) yakiwa na Kauli Mbiu isemayo PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA KATI”. yalifunguliwa rasmi na Waziro Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) siku ya Jumanne Oktoba 23, 2018 na yanatarajiwa kuhitimishwa siku ya Jumapili Oktoba 28, 2018.

MWISHO

Sunday, October 14, 2018

Wakala wa Mbegu Watakiwa Kushirikiana na Halmashauri Kutatua Changamoto Zinazo wakabili


 Mkurungenzi  Msaidizi wa Idara ya Usalama wa Chakula Bi Josephine  Amolo (wa pili kushoto)  akineshwa aina ya mbegu ya mahindi iliyozalishwa na kampuni ya mbegu ya Namburi walipotembelea kiwanda hicho wakati wa kukamisha  ziara ya kutembelea miradi ya kilimo na mifugo iliyopo mkoani songwe . wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha mbegu kinachomilikiwa na kampuni ya mbegu ya namburi wakiweka mbegu kwenye vifungashio tayari kwa kuingia sokoni.

Wakala wa Mbegu wa Taifa ASA wametakiwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya zinazozunguka mashamba ya uzalishaji wa mbegu ili kusaidia kupata soko la mbegu kupitia wakulima wa halmashauri hizo,kusaidia kulinda miundombinu ya mashamba yao na kupata huduma nyingie za miundombinu kwa urahisi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usalama wa Chakula Wizara ya Kilimo Bi Josephine Amolo  akimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara hiyo hivi karibuni wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya kilimo na mifugo mkoani songwe wakati wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani.

Akiongea baada ya kupata aelezo kutoka kwa meneja wa shamba hilo mkurugezi amesema  changamoto zinazowakabili wakala wa mbegu ASA zinaweza kutatuliwa kwa kushirikiana kwa karibu na Halmashauri zinazozunguka mashamba yao ya uzalishaji mbegu kwa kusaidia kuimarisha ulinzi wa maeneo hayo.

Amesema kwa kushirikiana na viongozi wa halmashauri itasaidia kuondoa tatizo la uingizaji wa mifugo katika maeneo ya uzalishaji wa mbegu,uchomaji moto kiholela katika mashamba ya megu unaofanywa na wananchi wakati wa kutafuta panya kwa ajili ya kitoweo na upatikanaji wa umeme utakaosaidia katika kuchakata mbegu.

Naye meneaja wa shamba la mbegu la Mbozi bwana Eliudi John  Msumi amezitaja changamoto nyingine  zikiwemo utegemezi wa mvua katika kilimo, ukosefu wa mtaji wa kutosha  na rasilimali watu kunachangia kwa kiasi kikubwa kuzalisha katika eneo dogo la hekt 943.3 kati ya hekta 3000 zinzofaa kwa kilimo.

Aidha Bwana Msumi amesema katika hekta 943.3 zinalimwa kwa ushirikiano wa makampuni ya mbegu ambayo ni Suba Agro,Meru Agrot, Namburi ,IFA seeds ,AGR Seeds na MAMS .
Amesema pamoja na changamoto zinazowakabila ASA lakini hali ya uzalishaji imekuwa ikiongezeka kila mwaka ambapo mwaka 2015/16 uzalishaji ulikuwa tani 2288 ikilinganishwa na msimu wa mwaka 2016/17 ambapo ulifikia tani 2667.5.