Thursday, November 29, 2018

BILIONI 4 KULIPWA KILA SIKU KWA WAKULIMA WA KOROSHO-MHE HASUNGA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari  tarehe 29 Novemba 2018 katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima.

Serikali imetangaza kuongeza kasi ya malipo ya wakulima waKorosho ili kufikia kiasi cha shilingi Bilioni nne (4) kila siku kwani kufanya hivyo zoezi la malipo kukamilika haraka.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 29 Novemba 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima.
Amesema kuwa zoezi hilo litaenda sambamba na kuongezwa kwa wataalamu kwa ajili ya kuongeza nguvu ya malipo huku akisisitiza kuwa wataalamu wengine tayari wamekuwa na uzoefu wa namna ya kuhakiki na namna ya kulipa tangu kuanza kwa zoezi hilo.
Mhe Hasunga alisema kuwa mikoa inayolima korosho ni mingi nchini hivyo wakati tathmini sambamba na malipo zikiendelea timu ya wataalamu wengine itaundwa kwa ajili ya kuanza kufanya tathmini katika mkoa wa Pwani na mikoa mingine inayolima korosho nchini.
Katika hatua nyingine amesema kuwa serikali imejipanga kuwatambua wakulima wote wa korosho nchini ili kurahisisha kuwahudumia na kuainisha tathimini mahususi ya wakulima hao nchini.
Kuwafahamu wakulima hao itaisaidia serikali namna ya kushirikiana nao na kuwasaidia ili wakulima hao waweze kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo.
Miongoni mwa changamoto ilizokutana nazo serikali katika zoezi la uhakiki ni pamoja na kutotolewa takwimu sahihi na Vyama vya msingi vya ushirika za wakulima wa korosho kwani takwimu hizo zinatofautiana na vyama vikuu vya ushirika.
“Jambo hili la takwimu kwenda kinyume linatupa uhakika kwamba kuna taarifa zilikuwa zinapikwa ili kumnyonya mkulima lakini changamoto zingine ambazo zimetukumba ni pamoja na uchache wa maghala kwani yaliyopo hayatoshi” Alikaririwa Mhe Hasunga
“Kuna changamoto za mgomo wa wapakuaji na wapakiaji wa mizigo, nasi kama serikali tutakuwa na kikao hivi karibuni na wasafirishaji ili kuhakikisha kuwa wanalipwa fedha zao haraka iwezekanavyo baada ya kupitia mikataba yao kujiridhisha jinsi walivyokubaliana” Alisema
Tayari vyama 163 vya wakulima wa korosho vimekwisha hakikiwa mpaka kufikia jana jioni tarehe 28 Novemba 2018 kati ya vyama 617 vinavyojihusisha na zao la korosho nchini.
Katika vyama hivyo vilivyohakikiwa tayari malipo yamevifikia vyama 97 ambapo wakulima 22,269 wameshalipwa huku kiasi cha korosho ambazo zimekwishalipiwa ni kilo 6,712,681 huku jumla ya Bilioni 22,151,00,000.8 zikiwa zimekwishalipwa.
Aidha, mpaka kufikia jana jioni tarehe 29 Novemba 2018 serikali imekwisha hamisha kiasi cha Tani 9,347.2 kutoka kwenye maghala makuu.
Pia Waziri Hasunga ameyataja matarajio ya serikali katika uzalishaji wa Korosho kuwa ni takribani Tani 245,495.8Wednesday, November 28, 2018

MHE HASUNGA AFANYA KIKAO KIZITO NA TIMU YA WATAALAMU OPARESHENI KOROSHO MKOANI MTWARAWaziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiongoza kikao kazi cha wataalamu mbalimbali wanaoshughulikia Opareshini ya ununuzi wa Korosho katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kilichofanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) kujadili mwenendo wa ununuzi wa zao hilo Leo tarehe 28 Novemba 2018.Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Leo tarehe 28 Novemba 2018 amezuru Mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi.


Katika ziara hiyo Mhe Hasunga atafatilia mwenendo wa ununuzi wa Korosho za wakulima katika kuhakikisha maelekezo ya serikali yanatekelezwa.


Mara baada ya kuwasili Mkoani humo Mhe Hasunga amekutana na wataalamu mbalimbali wanaoshughulikia Opareshini ya ununuzi wa Korosho katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na kufanya kikao kizito kilichofanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) kujadili mwenendo wa ununuzi wa zao hilo.

Tuesday, November 27, 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO AITAKA TARI KUSITISHA MAJARIBIO YA GMO


Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe leo tarehe 21 Novemba 2018 ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kusitisha mara moja utafiti na majaribio ya uhandisijeni (Genetic Modified Organism-GMO) yanayofanyika kwenye vituo vyake vya utafiti.
Aidha, Katibu Mkuu ameilekeza Taasisi hiyo ya TARI kuwa mabaki yote ya majaribio ya Uhandisijeni yateketezwe mara moja.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Taasisi hiyo kuanza kutoa matokeo ya utafiti bila kupata idhini ya serikali.
Siku za hivi karibuni Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kupitia kituo cha Makutupora imekuwa inaalika watu mbalimbali kwenda kuona matokeo ya utafiti wakati serikali haijaruhusu matumizi ya uhandisijeni nchini.

Monday, November 26, 2018

TUMEKUSUDIA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA KILIMO-MHE. HASUNGASerikali imedhamiria kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Kilimo ambapo Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara za Sekta ya Kilimo (ASLMs) na wadau wa kilimo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (Agricultural Sector Development Programme Phase Two-ASDPII). Katika utekelezaji wa ASDP II serikali imelenga kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo (mazao, mifugo na uvuvi) ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara na kuongeza pato la wakulima wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha na usalama wa chakula na lishe.Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 26 Novemba 2018 wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania inayofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam.Alisema Utekelezaji wa lengo hilo ni kuhakikisha kuwa Taifa linaendelea kujitosheleza kwa chakula; kuimarisha uchumi; kuwa kichocheo cha kukua kwa viwanda; na kuongeza ajira ambapo ili kufikia malengo hayo; Utekelezaji wa ASDP II utazingatia mnyororo wa thamani wa mazao ya kipaumbele ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Mhe Hasunga alisema kuwa Serikali itaendelea kuboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima na wafugaji na kwa bei nafuu.“Tumeanza na mbolea ambapo kwa sasa inaagizwa kwa pamoja na tumeondoa kodi na tozo nyingi katika mbolea ili ipatikane kwa bei nafuu. Kwa sasa changamoto kubwa imebaki kuwa gharama kubwa ya usafirishaji hasa kwa maeneo ambayo hakuna usafiri wa reli ambapo Serikali bado inalifanyia kazi suala hili” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa“Changamoto nyingine kama nilivyozitaja hapo awali tutaendelea kuzifanyia kazi na tunaomba wadau kupitia vyama vyenu na taasisi kilele kama Baraza la Kilimo, muendelee kutupa maoni yetu ya namna bora ya utatuzi na sisi tunaahidi kufanyia kazi maoni yenu”.Kuhusu Masoko ya mazao ya kilimo Mhe Hasunga alisema kuwa serikali inatambua changamoto za masoko, usindikaji, miundombinu ya umwagiliaji na miundombinu mingine kwa ajili ya mifugo na uvuvi, upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakati na kwa bei nafuu, uhaba wa maafisa ugani, kero za kodi na tozo mbalimbali, wingi na mwingiliano wa taasisi za udhibiti huku akiahidi kuendelea kuzitafutia ufumbuzi.“Baadhi ya kero hizi zimeshaanza kufanyiwa kazi. Mifano michache ni kuhusu tozo na kodi ambapo Serikali imeondoa kodi na tozo nyingi katika sekta ya Kilimo na bado tunaendelea kufanya maboresho katika eneo hilo.” AlisemaAidha, alisema kuwa Wizara ya Kilimo inatambua mahusiano ya moja kwa moja kati ya Sekta ya Viwanda na ile ya Kilimo na pia changamoto zilizopo.“Pamoja na dhamira ya Serikali iliyokuwepo katika kuweka mazingira mazuri ya biashara, ACT kama sehemu ya timu ya Kikosi Kazi Cha Taifa Cha Kuishauri Serikali Kuhusu Masuala ya Kodi, imekuwa ikitekeleza jukumu hilo bila kuchoka ambapo kwa kupitia ushauri huo, katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 na 2018/2019 Serikali imepunguza kodi na tozo nyingi sana katika sekta ya kilimo” Alisisitiza Mhe HasungaAlisema kutokana na jitihada hizi za ACT katika kuona kuwa kilimo kinakuwa moja ya ajenda kubwa kitaifa, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imekubali kuwa na makubaliano maalumu na ACT (Memorandam of Understanding – MoU) kwa lengo la kuifanya sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.Warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo yenye kauli mbiu isemayo“Kilimo na Maendeleo ya Viwanda Tanzania”  itafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 26-27 Novemba 2018 ambapo wadau wa sekta ya Kilimo katika maeneo mbalimbali ya mnyororo wa thamani yaani kuanzia wazalishaji (wakulima, wafugaji na wavuvi), wasindikaji, watoa huduma mbalimbali kama wasafirishaji na wauza pembejeo, wafanyabiashara ya mazao, wasindikaji ikiwa na mada mbalimbali zenye kuakisi juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuwa na Uchumi wa Viwanda ifikapo 2015.

MHE HASUNGA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MOROGORO ASISITIZA UMUHIMU WA MBEGU BORA

Imebainika kuwa malighafi nyingi zinazozalishwa kwa ajili ya viwanda nchini zinatokana na sekta ya kilimo ambayo inategemewa na watanzania kwa zaidi ya asilimia 75.


Hayo yamebainishwa tarehe 24 Novemba 2018 na Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Mbegu (ASA) katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.


Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipambanua katika usimamizi madhubuti wa ujenzi wa viwanda hivyo wananchi wanapaswa kuzalisha kwa wingi mazao mbalimbali katika sekta ya kilimo kwani uhai wa viwanda vingi vinategemea zaidi sekta ya kilimo.

Alisema kuwa Wizara ya kilimo itasimamia kwa weledi uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzalisha mbegu bora na kwa wingi ili wakulima waweze kunufaika katika uzalishaji wenye tija ili kuondokana na uzalishaji wa mazao kwa ajili ya chakula pekee badala yake kuzalisha kwa tija kilimo cha kibiashara.


“Katika viwanda tutakavyozalisha zaidi ya asilimia 60 ya malighafi zitakazotumika zinazalishwa hapa nchini, hivyo tunawajibu wa kutoa malighafi zinazotosheleza viwanda tunavyovianzisha” Alikaririwa Mhe Hasunga

Alisema kuwa wafanyakazi wote wa Wakala wa Mbegu (ASA) wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa kwani ndio silaha pekee itakayowafanya waweze kuzalisha mbegu nyingi kwa manufaa ya mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.


Alisema kuwa serikali ina mpango kabambe wa kuimarisha sekta ya kilimo nchini kitakachopelekea kupata chakula cha kutosha, kuongeza tija katika uzalishaji na kuongeza thamani ya mazao hayo.


“Huwezi kuwa na viwanda mpaka uanzie kwenye kilimo na kilimo hakiwezi kustawi bila kuwa na mbegu bora za mazao hivyo wakala wa mbegu ni Taasisi muhimu nchini kwenye sekta ya kilimo” Alisisitiza Mhe Hasunga


Aidha, Mhe Hasunga alisema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakilima bila kufuata taratibu za kilimo hivyo wataalamu mbalimbali wa kilimo nchini wanatakiwa kufanya kazi zaidi kwenye maeneo ya wakulima kwa kufika mashambani ili kuwaongezea weledi na ujuzi wakulima kote nchini.